fbpx

Elon Musk afuta kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook baada ya kujaribiwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Mambo si mazuri kabisa kwa upande wa Facebook baada ya kukumbwa na kashfa inayopelekea watu kuanza kuukacha mtandao huo wa kijamii wenye watumiaji wengi ulimwenguni.

Mara tu Bw. Brian Acton ambaye ni mwanzilishi mwenza wa WhatsApp (hivi sasa WhatsApp ipo chini ya Facebook baada ya kununuliwa kwa $16bn) kuanzisha kampeni ya kufuta akaunti ya Facebook (#DeleteFacebook), sasa suala hilo ni maarufu sana kwenye Twitter inaonekana kupata mwitikio kutoka kwa watu wengi.

INAYOHUSIANA  Serikali ya Uchina na magari yanayotumia umeme

Elon Musk ni mmoja wa watu ambao wamefuta kurasa za SpaceX na Tesla zilizokuwa zimeshaidhinishwa (verified) baada tu ya mtu mmoja kumwambia “Afute kweli kama yeye ni mwanaume”.

kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook

Elon Musk: Alichokijibu kwenye Twitter baada ya kujaribiwa iwapo anaweza akafuta kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook.

Ni kitu rahisi sana kufuta ukurasa kwenye Facebook lakini ukweli ni kwamba Facebook wenyewe wamefanya imekuwa ngumu sana kuondoa kabisa ukurasa husika hata mara baada ya kile kipindi ambacho unaruhusiwa kurudisha tena ukurasa wako hewani kupita.

kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook

Kufutwa kwa kurasa za SpaceX na Tesla: Hiki ndio utakachokiona baada ya kujaribu kutafuta ukurasa wa SpaceX/Tesla kwenye Facebook.

Elon Musk ameonekana mtu wa kutojali uwepo wa kurasa za mitandao ya kijamii kuhusu kile ambacho kampuni zilizopo chini yake zinazalisha. Pengine kujiamini huko kunatokana na alivyoweza kuibadilisha Tesla iliyokuwa ikionekana kampuni ambayo inaishia na kuibadilisha kabisa kwa kuifanya kuwa moja ya makampuni yenye uwekezaji mkubwa kwenye teknolojia.

INAYOHUSIANA  Facebook yashindwa kesi kuzuia kushtakiwa

Ni rahisi/vigumu kiasi gani kufuta ukurasa wa kwenye Facebook ambao unatumia/ulitumia muda mwingi kuujenga na kufikia mpaka hapo ulipo na ukizingatia kuna kashfa iliyoikumba Facebook?

Vyanzo: Gadgets 360, Vox

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|