fbpx

Facebook Messenger: Jinsi ya kutafuta ujumbe uliotoweka

0
Sambaza

Facebook Messenger iliyo katika umaarufu wake kwa kuwa na vionjo vingi ndani yake kwa kumfanya yule anayetumia njia hiyo ya kufanya mazungumzo kwa njia ya maandishi kutoona tofauti iwapo atatumia kwenye simu/kompyuta.

Ni jambo la kawaida sana mtu kutokuwa na tabia ya kufuta msururu wa mazungumzo kwenye Facebook kwa njia ya Messenger lakini unaweza ukajikuta kwa bahati mbaya au bila kujua mazungumzo yako na mtu fulani/kundi hayaonekani na kuamini kuwa mazungumzo hayo huenda umeyafuta.

Kama ni una uhakika kuwa umefuta mazunguzo hayo basi itakuwa ni ngumu sana kama si kutowezekana kabisa kuweza kuyapata tena mazungumzo hayo na iwapo una uhakika kuwa hukufuta basi tambua kuwa mazungumzo hayo yapo ila tu ni hujui yalipojificha 😆 😆 😆 .

INAYOHUSIANA  Kenya nayo yafikiria kudhibiti WhatsApp na Skype

A. Namna ya kutafuta kile kilichopotea/kujificha kwenye Facebook Messenger.

Katika kufanikisha kupata yale mazungumzo yako ambayo usingependa kabisa uyapoteza haihitaji uwe na ujuzi wa masuala ya teknolojia lakini cha msingi ni kuwa mtundu wa kucheza na sehemu ile ambayo jumbe zako za Facebook zinahifadhiwa:-

  1. http://signaturemassagekcmo.com/about-us/dawn-chandler-cropped/ Fungua Facebook Messenger. Kamwe haitawezekana kujua kama unaweza kupata kile ambacho unafikiri umekipoteza kwa bahati mbaya kwenye Faceook Messenger iwapo hutoanza na hatua hii.

    app ya messenger

    Facebook Messenger: Uwanja wa mbele kwa jumbe zote ambazo zinaonekana waziwazi na kwa urahisi.

  2. http://tpqwikstop.com/saukville/lunchtime-love/ Bonyeza sehemu ya mpangilio ndani ya Facebook Messenger. Ukiwa ndani ya Facebook Messenger ambapo unaona zile jumbe zote ambazo hazijajificha, angalia upande wa kushoto juukidogo pembezoni kisha bonyeza hapo. Menyu ndogo itatokea na utachagua archived messages.

    Facebook Messenger: Ndani ya kipengele cha archieved messages ndio utaweza kuona zile jumbe zote ambazo hazionekani kwenye uso wa mbele kwenye Facebook Messenger.

B. Utafanyaje ili uweze kuficha mazungumzo fulani kwenye Facebook Messenger?

Njia ya kutumia ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kwenda yule mtu ambaye unataka mazunguzo kati yako na yeye/kikundi fulani yasionekane kwenye Messenger yako na kubofya kwenye mpangilio (upande wa kulia) pembeni kidogo ya mtu ambaye hutaki kuona mazungumzo yenu.

Ukiweka msururu wa mazunguzo yenu kwenye orodha ya zile jumbe ambazo zimefichwa basi utakuwa na uhakika wa mtu mwingine kutoweza kuona kwa urahisi msururu wa mazungumzo yenu iwapo ataingia kwenye akaunti yako ya Facebook.

Mazungumzo yaliyofichwa yanawezekana kabisa kuyafuta lakini cha kukumbuka na kuzingatia ni iwapo utaamua kufuta kabisa mazunguzo hayo basi ujue kuwa hutaweza kuyaona tena kiurahisi kama ilivyokuwa hapo awali.

Vyanzo: Wiki How na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.