WhatsApp ni njia rahisi sana ya kuwasiliana na ndugu jamaa na hata marafiki. Ndani ya mtandao huo kuna mambo mengi kadha wa kadha.
Hivi karibuni mtandao huo uliongeza huduma nyingingine ambayo inajulikana kama ‘Live Location‘ katika huduma yake ya kutambua maeneno (location).
Sasa Live Location Ni Kitu Gani?
Kwa haraka haraka ni kwamba ‘Live Location’ ni huduma ambayo itamuwezesha rafiki yako kujua sehemu uliyopo (kwa kutumia ramani uliyomtumia) kwa muda wote ambao umeutegesha.
Kwa mfano unaweza ukawa Tabata na kisha uka’share’ live location yako na rafiki yako yoyote labda kwa muda wa saa nane (chaguzi za muda yako mengi). Hii inaamaanisha rafiki yako ataweza kujua uko wapi muda wote huo mpaka saa nane zikatike.
Hii inamaanisha kwamba hata kama ukihama sehemu (mf. Tabata kwenda Kariakoo) bado rafiki yako atajua sehemu kamili ulipo.
Kama ukiniuliza mimi ntakuambia kabisa kuwa hii ni huduma ya aina yake, hebu fikiria kama mnapanga kukutana na mtu hii inaweza ikatatua yote hayo bila ya mtu kuanza kuuliza maswali kadha wa kadhi ili kukufikia. Kinigine ni nzuri katika suala zima la kuhakikisha kuwa mtu anafanya kile ambacho mmekubaliana mathalani kuhakikisha mtoto anaenda kupata mfunzo ya ziada (tuition) kama inavyotakiwa, n.k.
Jinsi Ya Kutumia Live Location
Ingia katika mtandao wako wa WhatsApp kama kawaida, katika sehemu ambayo unaweza ku’Attach’ mafaili mbali mbali na kisha chagua ‘Location’.
Hii ikifunguka utaona kuna chaguo la ‘Share Live Location’ ambalo unaweza kulichagua ili kuanza mchakato wote. Mpaka hapo nadhani utakua umeelewa fika kipengele hiki na jinsi ya kukitumia.
Hebu fikiria katika makundi ya WhatsApp (WhatsApp Group) kipengele hiki kinaweza kikawa ni msaada mkubwa. Fikiri ‘Group’ la watu 250 lilivyo kubwa lakini mtu mmoja anaweza aka’Share Live Location’ kwa kikundi kizima ili kuwezesha kukutana katika vitu kama sherehe, n.k.
Ili kufurahia duduma hii inakubidi uwe na sasisho jipya (Update) kabisa la WhatsApp.
Ningependa kusikia kutoka kwako, kwa maono yako mwenyewe unahisi kipengele hiki kingesaidia mambo gani? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.
Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!