Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sayansi, simu, Teknolojia

Fikiria Simu Bila Ya Betri, Teknolojia Hii Ipo Katika Hatua Zake Za Kwanza!

fikiria-simu-bila-ya-betri-teknolojia-hii-ipo-katika-hatua-zake-za-kwanza

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Ni wazi kuwa kuna mambo mengi ambayo yanatushangaza katika teknolijia na sayansi. Najua ni wengi wameshawahi fikiria kama kutaweza kuwa na simu ambayo haina betri. Pengine huu ndio mwanzo wa kuliwezesha hilo.

Simu zetu zikiwa hazina uwezo mzuri wa betri inakua ni tabu sana, hivi unajua kwamba asilimia kubwa ya wanaotumia simu janja huwa wanatembea na chaja za simu zao wakiwa katika safari zao za hapa na pale.

INAYOHUSIANA  Miaka 40 ya Apple; Mambo 5 ambayo pengine huyajui
Timu Nzima Nyuma Ya Simu Isiyotumia Betri

Watafiti toka chuo kikuu cha Washington wameandaa simu ambayo haitumii betri hii ikiwa ni moja kati ya harakati za kuhakikisha kuwa dunia inapata simu ambayo haina betri hivyo kuishiwa chaji itakua ni mtihani.

Lakini ukiangalia simu hii ambayo watafiti wamekuja nayo haina sura ya kawaida kama simu zingine tulizozizoea. Hii kidogo ina umbo la kipekee kwani ipo kama ni sakiti tuu.

Simu Isiyotumia Betri

Watafiti hao wanasema kuwa hapa kinachofanyika ni kwamba mfumo wa uzalishaji unabadilish audio iliyo katika mfumo wa analogi na kuupeleka katika digitali ili kifaa kiweze kutafsiri.

INAYOHUSIANA  Samsung yaweka rekodi kwa kupata faida ya mamilioni ya dola ndani ya siku moja

Hii inamaanisha kuwa kwa sasa kifaa hicho kitachukua muda mrefu katika kutafsiri mambo hivyo na mtumiaji nae  atatumia muda mwingi wakati anatumia. Kwa mfano mtumiaji akisema ‘Halo’ itambidi asubiri sekunde kadhaa kifaa kitafsiri hilo neno, kitume neno kwa mtu husika, alafu krudishe majibu.

Jionee Video Yake Hapa

Lakini usitegemee kuona simu ya namna hii hivi karibuni kwani hizi ni hatua za mwanzo mwanzo kabisa. Ukiachana na hayo ni kwamba mambo kama haya yanachukua muda sana, Mpaka ifikie unaona iPhone au Samsung inakua inatumika bila ya kuwa na betri si jambo dogo.

INAYOHUSIANA  Facebook M: Msaidizi Anayefanya Kazi Kama Ile ya 'Siri' au 'Google Now'

Ningependa kusikia kutoka kwako, wewe hili unalionaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com