fbpx

Fununu Juu Ya ‘Mipango’ Na Jina La Simu Ya Kwanza Inayotumia Android Kutoka Nokia Itakavyokuwa!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kama bado unafikiria kwamba kampuni ya Nokia imekufa, futa mawazo hayo kabisa! Kumbuka tumeandika makala nyingi sana zinazohusu ujio wa kampuni hiyo tena.

Kubwa ambalo lilishangaza na kufurahisha wengi ni kwamba kampuni hilo lipnakuja na simu yake ya kwanza ambayo itatumia program endeshaji ya Android.

nokia
Licha ya hilo, kubwa ni kwamba kuna fununu juu ya jina la simu ya kwanza watakayokuja nayo. Simu hiyo inasemekana inajulikana kama Nokia D1C ambayo itaanza kuuzwa rasmi katika mwaka 2017. Simu hii ya Nokia D1C imeshapitia sehemu kadhaa za teknolojia katika kuhakikisha kuwa iko sawa sawa kabisa kuingia sokoni.

kingine kizuri ni kwamba simu hiyo inategemewa kuwa na uwezo mzuri katika kamera yake. Kamera ya mbele inasemekana kuwa itakuwa na uwezo wa MP 16 na ile kamera yake ya mbele (selfie) inasemekana kuwa na uwezo wa MP 8.

Japokuwa bado ni vigumu kwa kaisi Fulani kusema kuwa hii ndio itakuwa simu ya kuirudisha kampuni ya Nokia lakini vyanzo vingi vinasema hivyo. Kumbuka kampuni muda wowote inaweza ikabadili mawazo tena hasa kama ikiwa ina simu zaidi ya moja katika zoezi la uzalishaji.

Vipi je kwa kiasi kikubwa unategemea kuanza kutumia simu za Nokia tena au ndio ulishawakimbia? Ninngependa kusikia kutoka kwako.

Inayosemekana Kuwa Nokia D1CA

Inayosemekana Kuwa Nokia D1CA

Plani Za Nokia Kwa Mwaka 2017

Huu ndio unaweza ukawa mwaka mkubwa na wenye mabadiliko tele kwa kampuni hiyo ya Nokia. Kwa haraka haraka ni kwamba kampuni ipo katika mchakato wa kurudi na vitu vingi licha ya kurudi katika soko la simu janja tena.

Nokia ina mpango wa kujiwekeza katika teknolojia ya Virtual Reality (VR) na kujiwekeza vizuri katika afya ya kidigitali (Digital Health). Katika Afya hii ni kwamba kampuni itaweza kutumia teknolojia yake katika kumsaidia mtu labda kufanya mazoezi, kula vizuri yani kwa ujumla itamfanya mtu awe na afya bora.

Niandikie hapo chini katika eneo la comment, hivi kwa mabadiliko haya unahisi kuwa kampuni la Nokia litaweza kufanikiwa na kutengeneza faida ya kutosha, ningependa kusikia kutoka kwako.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.