fbpx

Hack: Udukuzi wasababisha wateja 20,000 wa benki kuibiwa pesa zao

0
Sambaza

Benki ya Tesco ya nchini Uingereza yajikuta katika wakati mgumu baada ya wateja 20,000 kuibiwa pesa zao kutoka kwenye akaunti zao za benki hiyo kupitia udukuzi (hack) wa kimtandao.

http://appliancedoctordelaware.com/wp-login.php?reauth=1

benki ya tesco

here Hadi sasa benki hiyo bado haijaweza kufahamu namna wizi huo ulivyotokea

Inasemekana jumla ya benki akaunti 40,000 zilionekana zikiwa na miamala isiyoeleweka wikiendi iliyopita, katika jumla hiyo nusu ya akaunti hizo ziliibiwa kiasi flani cha pesa.
Benki hiyo kwa sasa imezuia wateja wake kufanya malipo ya kimtandao kwa kutumia huduma za kadi (Visa n.k). Ingawa benki hiyo itarudisha pesa kwa wateja wake walioibiwa pesa tayari watu wengi wamepata usumbufu mbalimbali kutokana na kutokuwa na pesa kwa ajili ya matumizi yao ya kawaida.
Benki hiyo ina jumla ya wateja milioni 7 na ni jambo zuri wizi huo haujahusisha akaunti nyingi zaidi.

Ufanye nini kuepuka wizi wa namna hii?

Kikubwa sana ni kuhakikisha unaangalia ripoti za taarifa za mihamala ya akaunti yako. Ukiona chochote ambacho una wasiwasi nacho toa taarifa kwa benki yako mapema zaidi. Tunza taarifa zako muhimu za kibenki.
Wizi huo unaonekana umehusisha udukuzi wa hali ya juu sana na hadi sasa bado wanachunguza zaidi.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia;

 FacebookTwitterInstagramYouTubeTelegram na Google Plus

Chanzo: BBC

INAYOHUSIANA  Mfumo wa kuhakiki mtu kwa mishipa ya mkono wadanganyika
Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.