fbpx

Hili ndio toleo la Nokia 7

1

Sambaza

Simu za Nokia ambazo zinaendeshwa na programu endeshaji ya Android zinaendelea kupendwa na kwa sehemu zingine kama Uchina zimejichukulia umaarufu mkubwa.

Matoleo mengi ya Nokia yapo madukani lakini Nokia 6 ambayo ilizinduliwa huko Uchina na kuacha historia ambayo itakumbukwa kwa miaka mingi tu na kampuni husika, soma zaidi click here hapa.

Hii ni Nokia 7 na ina haya yafuatayo:-

buy Premarin online cheap Kioo & Kamera. Kioo chenye ukubwa wa inchi 5.2, ubora wa picha ukiwa 1080*1920 pixels lakini ikiwa inakingwa Corning Gorilla Glass 3 isipate madhara inapoanguka. Upande wa kamera ya nyuma ina MP 16 na ile ya mbele ina MP 5 iliyotengenezwa na Zeiss ikiwa na LED flash mbili.

INAYOHUSIANA  Simu janja ya kwanza yenye "V" mbili

http://understandingsin.com/wp-login.php?action=jetpack-sso Programu endeshi & Prosesa. Imewekwa Android 7.1 lakini ikiwa na uwezo wa kuhamia Android 8 (Oreo). Prosesa ambayo ipo kwenye Nokia 7 ile maarufu na inayotumiwa na makampuni mengi tu, Qualcomm SDM630 Snapdragon 630 kasi yake ikiwa Octa-core 2.2 GHz.

toleo la Nokia 7

Nokia 7 inatumia laini 2 za simu na ikipatikana katika rangi mbili; Nyeupe na Nyekundu.

RAM & Diski uhifadhi. Moja ya kiungo muhimu cha kufanya simu kutokwamakwama ni RAM, Nokia 7 ina GB 4 na GB 64 uhifadhi wa ndani kwenye simu lakini ikiwa na uwezo wa kukubali uhifadhi wa ziada wa mpaka GB 256.

Betri & Sifa nyinginezo. Hapa kuna betri yenye 3000 mAh aina ya Li-ion ambalo halitoki; linadumu kwa chaji saa 340 ukitumia kwenye intateti tu, saa 15 (kuongea+intaneti), saa 85 ukitumia kusikiliza muziki peke yake.

Nokia 7 ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole iliyowekwa upande wa nyuma, kuna redio, WLAN, Bluetooth, sehemu ya kuchomekea spika za masikioni, GPS, NFC.

toleo la Nokia 7

Nokia inakubali teknolojia za mawasilaiano kama vile GSM / CDMA / HSPA / EVDO / LTE.

Nokia 7 ipo madukani muda mrefu tu na kwa makadirio ni zaidi ya Tsh. 655,00. Nokia 7 Plus, 7.1, 7.1 Plus zipo na zinawika kweli. Uchambuzi wake utakuja katika siku za usoni.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|