fbpx

Huduma ya 5G ya kwanza kwa watu wote yawashwa kwa majaribio! #Australia

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kampuni kubwa ya mawasiliano ya Telstra ya Australia mwanzoni mwa wiki hii imewasha teknolojia ya 5G ya majaribio yenye kasi zaidi kwa njia ya Wi-Fi.

Kampuni hiyo inakuwa ya kwanza kuwasha teknolojia ya 5G duniani na itapatikana bure katika michezo ya jumuiya ya madola (GC2018) itakayofanyika nchini humo kuanzia April 04 mpaka April 15 mwaka huu.

5G ya kwanza

HUDUMA YA KWANZA YA 5G KWA WATU WOTE: Australia, kupitia mtandao wa Telstra, imekuwa ni nchi ya kwanza kuwa na huduma ya majaribio kwa umma.

Teknolojia ya 5G itapatikana katika Pwani ya Gold coast, Queenslands ambapo michezo ya jumuiya ya madola itafanyika na wageni watakaohudhiria katika michuano hiyo watafurahia kupata intaneti ya bure na kusaidia kujaribu teknolojia mpya ya 5G.

Huduma ya 5G ya kwanza kwa umma: Mtandao wa Telstra

Hata hivyo hakuna bado simu janja, Tablet au vifaa vinginevyo ambavyo vinaruhusu matumizi ya 5G. Kampuni ya Telstra imeweka idadi ya vituo vya Wi-Fi vinavyowezesha 5G ili kuweza kupima zaidi miundo mbinu yake mipya.

INAYOHUSIANA  Samsung Imesema Itazidi Kuwa Namba 1 Kwa Miaka Mingine 10!

Telstra imetoa tahadhari kwamba kasi ya intaneti hiyo itatofautiana kulingana na vifaa vya watumiaji, umbali wa WiFi na mtumiaji na wingi wa watumiaji waliounganishwa kwenye Hotspot moja.

Wakati Telstra imeanza rasmi majaribio ya 5G huko Australia, Marekani kampuni za mawasilino za AT&T na Verizon zipo kwenye maandalizi ya kuanza teknolojia ya 5G.

AT&T imepanga kuanza teknolojia ya 5G katika miji 12 Marekani wakati Verizon wanashirikiana na Samsung kwa kuanzia huko Sacramento, California baadae mwaka huu.

INAYOHUSIANA  Windows 10; Kwa nini ni bora zaidi na uipate kabla muda wa BURE kuisha! #DoMore

Kwa sasa teknolojia ya 4G ndio inayotamba kwa kuwa na kasi zaidi na bado haijaenea katika maeneo mengi duniani.

Kampuni kadhaa za simu zikiwemo samsung na Apple zimeahidi kutoa simu zenye teknolojia ya 5G kufika mwaka 2019.

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.