fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Tanzania Teknolojia Tigo

Huduma za TigoPesa na M-Pesa vyapata vyeti vya ubora

Huduma za TigoPesa na M-Pesa vyapata vyeti vya ubora

Spread the love

Miamala kwa njia ya simu ni jambo la kawaida sana katika nchi nyingi tu za Afrika na huduma za M-Pesa na TigoPesa zinazotolewa na Tigo na Vodacom Tanzania zimepewa vyeti kuidhinishwa kuwa huduma bora za kifedha.

HUduma za kifedha zinatumika sana na kuwa ajira kwa wengine, kurahisisha miamala (kutuma/kupokea pesa) na hata kuongea pato la taifa kwa njia ya ulipaji kodi. Mwaka 2018 Aprili 13 utaingia kwenye historia ya Tigo na Vodacom Tanzania baada ya huduma ya TigoPesa na M-Pesa kutimiza vigezo vyote kwa asilimia 100 hivyo kutambulika kimataifa kama huduma bora.

Huduma za TigoPesa na M-Pesa

Kuna akunti za kufanya miamala ya kifedha zaidi ya 690 milioni duniani kote jambo linalowezesha watu kuhifadhi pesa zao na kuweza kupata huduma ya kifedha kwa mapana zaidi.

Undani wa TigoPesa na M-Pesa kupewa cheti cha ubora.

Katika kukidhi viwango vya mtoa huduma za kifedha anayetambika na GSMA Mobile Money ni laziam awe amechunguzwa na kuthibitika ni za kuaminika, kuna uwazi na usalama wa fedha za wateja wao. Vigezo vyote hivyo ni lazima mtoa huduma apate alama 100 katika kila kigezo kilichowekwa na GSMA Mobile Money.

Huduma za TigoPesa na M-Pesa

Tigo na Vodacom ndio mitandao ambayo inaongoza zaidi kwa kufanya miamala ya kifedha kwa njia ya simu. Ukiunganisha wateja wa Tigo na Voda ni karibu ya nusu ya wateja mitandao ya simu wote nchini Tanzania.

Makampuni mengine yaliyopata cheti cha ubora kutoka GSMA Mobile Money ni pamoja na Orange Côte d’Ivoire, Safaricom (Kenya) na Telenor Microfinance Bank Ltd. (Easypaisa Pakistan).

Kwa uthibititsho huu unaziweka TIgoPesa na M-Pesa katika nafasi nzuri kuzidi kuaminiwa na wateja wake na pengine hata kuleta mengi mazuri kwa wateja wa huduma hizo.

Vyanzo: TIgo, Dignited

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] post Huduma za TigoPesa na M-Pesa vyapata vyeti vya ubora appeared first on TeknoKona Teknolojia […]

  2. […] zilizoenea barani Afrika kwa wingi na kufanya kuwa na soko zuri barani humo lakini halikadhalika Tigo Tanzania nao wamekuwa wakijidhatiti ili kuweza kuendelea kufanya vizuri katika soko lenye ushindani na hatimae wasipoteze […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania