fbpx

IBM yainunua Red Hat kujiimarisha

0
Sambaza

Moja ya makampuni nguli kwenye ulingo wa teknolojia imeamua kutanua wigo wa kuvutia zaidi kwa kununua kampuni inayofahamika kwa kuwa na usalama lakini haijafungua programu zake nikimaaanisha Red Hat.

go

Siku si nyingi zilizopita IBM imeweka wazi kuwa sasa Red Hat ipo chini yake na kabla ya hapo wamekuwa wakishirikiana kwa miongo miwili katika kujiweka vizuri kwenye mambo ya teknolojia pamoja na wateja wake.

Kwanini IBM imeinunua Red Hat?

IBM imeamua kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa kutokana na kwamba imeona umuhimu wa kuhifadhi data mahali ambapo sio rahisi kufikika na pasipojulikana (cloud). Sababu ya pili ni kuweka nguvu kwenye utengenezaji wa programu ambazo hazijifungi kwa lugha rahisi mtaalam yeyote anaweza kuziboresha (open source).

Red Hat

Programu ambazo zinakuwa na uwezo wa kuandikwa/kuboreshwa na mtu zaidi ya mmoja huwa zinasaidia ufanisi wa kitu husika.

Kwa kiasi gani?

Kiasi cha $34bn kimetumika kununua kampuni hiyo ambayo imejikita katika utengenezaji wa programu za bure lakini pia ambazo zinaweza kuboreshwa na mtu yeyote ambae ana ujuzi na uwandishi wa programu.

Matarajio baada ya IBM kununua Red Hat.

Kwa uwekezaji/maamuzi ambayo IBM imeyafanya inatazamiwa nguvu kuongezeka katika utengenezaji wa programu ambazo zinashirikisha watu wengi kuziboresha lakini pia kuongeza uaminifu kwa wateja wao kuweka data zao “Mawinguni”; buy orlistat (xenical) ni 10%-20% ya wateja wa IBM ndio wanahifadhi vitu vyao sehemu ambayo wanaweza kuvipata muda wowote.

Komyuta zenye uwezo wa hali ya juu kwenye kutuza data: IBM itakuwa na uwanja mpana zaidi wa kuweza kuhifadhi vitu vya wateja wao.

Kutokana na ukuaji wa teknolojia makampuni mengi tuu yanahamisha mfumo wa utunzaji wa vitu kwenye sehemu ambayo haitakuwa rahisi kufikika/kudukuliwa lakini pia gharama nafuu zinazohusina na suala zima usalama.

Vyanzo: Engadget, ZDNet, Wired

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.