fbpx

iPhone XR ni simu janja ya wengi

0

Sambaza

iPhone XR ni simu mojawapo kati ya 3 zilizozinduliwa na Apple Sept. 12 2018 na wengi wakifurahia ujio wa simu hizo zenye kutofautiana kidogo sana hasa iPhone XS na XS Max.

Kati ya simu zote 3 kutoka Apple kwa mwaka huu (2018) iPhone XR ndio simu ya bei ya rahisi kulinganisha na nyingine ambazo zilitambulishwa siku hiyo. buy Depakote online in uk Watu wengi wamethubutu kutabiri kuwa iPhone XR itakuwa ni “Simu ya wengi”.

iPhone ambayo inaelezwa kutokuwa ghali inajitofautisha na wenzake katika maeneo makuu matatu:

cheap xenical orlistat Muonekano: Simu hiyo imefunikwa na alminium pamoja na kioo tofauti na wenzake ambao wanachuma ambacho hakipati kutu.

orlistat tablets usa Kamera: Toleo la XR halina kamera mbili za nyuma kama ilivyo kwenye iPhone XS na XS Max.

3D Touch. Kama unapendelea iPhone ambayo ina teknolojia ya 3D Touch basi si kwa simu hiyo kwani kitu hicho hakijawekwa huko.

iPhone XR

iPhone XR ndio toleo ambalo linapatikana katika rangi nyingi tofauti kuzidi wenzake. Katika kuzuia simu kutoingia maji inatumia teknolojia ya IP67.

Mbali na kuwa na sifa za utofauti na wengine ambao walizinduliwa siku moja ni vyema ukafahamu mambo mengineyo yanayoihusu simu yenyewe.

INAYOHUSIANA  Kamera 3 kwenye Samsung Galaxy F

Kipengele

Maelezo

Aina/Urefu wa kioo Kioo chake ni LCD na kina urefu wa inchi 6.1. Pia ina umbo la herufi “V” kwa juu.
Kipuri mama/Programu endeshi A12 Bionic kama ilivyo kwenye iPhone XS na XS Max. Inatumia programu endeshi toleo 12 (iOS 12).
Kamera Kwa ujumla kuna kamera mbili, ile ya nyuma ikiwa na MP 12 na ya mbele MP 7.
Uwezo wa betri

Haijabainika wazi kabisa nguvu ya betri kwenye simu husika lakini inaekezwa inadumu na chaji kwa saa moja na nusu zaidi ya iPhone 8 Plus.

Kadi za simu

iPhone XR ina kubali kadi mbili za simu (toleo maalum) lakini mojawapo ya laini ipo katika mfumo wa eSIM.

Rangi

Kwa ujumla simu husika inapatikana katika rangi sita (6) tofauti ikiwemo Nyekundu, Nyeupe, Bluu, Nyeusi.

RAM/Memori ya ndani

RAM yake ina ukubwa wa GB 3 na kwenye diski uhifadhi zipo zenye GB 64, GB 128 na GB 256.

INAYOHUSIANA  Xiaomi yaendelea kukua kwa kasi

Kuanza kupatikana kwake ni mpaka mwezi Oktoba na bei inayofahamika ni ya ile yenye GB 64 ikiuzwa kwa $749|Tsh. 1,722,700.

Vyanzo: The Verge, Medium

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.