Milipuko ya simu janja za Samsung Galaxy Note 7 zimefanya watu wengi kujiuliza maswali mengi zaidi kuhusu usalama wa betri za simu.
Teknokona kama mdau wa teknolojia imeliona hili na kuamuua kuliangalia suala hili kwa undani zaidi. Je, unajua ni jinsi gani betri za simu zinavyofanya kazi na kwanini nyingine hulipika? Pata kujua
Betri ni nini?
Ni mchanganyiko wa kemikali mbalimbali mbazo zikitumiwa huzalisha umeme. Betri hizi huifadhiwa katika kifaa maalum. Betri hizi hutengengezwa kwa Anode, Cathode pamoja na elektrolaiti.
Simu janja nyingi pamoja na vifaa vya kielektrnoniki hutumia betri zenye lithium ambayo yameundwa kwa madini ambayo huwezesha elektroni kusafiri kutoka upande wa chaji chanya(+) kwenda chaji hasi(-). Kwa lugha rahisi tunasema kutoka Anode kwenda Cathode.
Betri kutokaa na chaji muda mrefu
Hili limekuwa ni tatizo sana kwa simu janja lakini kutokaa na chaji muda mrefu kunatokana na ukubwa/udogo wa betri yenyewe. Betri aina ya Lithium inazalisha umeme kwa kiasi cha Watt 150 kwa kiogramu (150 Watt-hours/Kg) na kiwango hicho ni baada ya kufanyiwa maboresho miaka ya ’90 – yaani kabla hata ya uwepo wa simu janja 🙂  .
Na kila betri inawastani wa idadi za kuishiwa chaji na kuchajiwa…baada ya kuisha chaji na kuchajiwa mara nyingi zaidi moja kwa moja betri linapoteza uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu kama ilivyokuwa mwanzo.
Kama simu yako inatumia betri nene basi itahifadhi umeme muda mrefu na kama simu yako inatumia betri nyembamba basi itakuwa inahifadhi chaji muda mfupi (kama simu janja zetu). – ila siku hizi makampuni mengi kama Apple na Samsung wanajitahidi kufanya vitu ndani ya betri viwe vidogo sana bila kuathiri sana kiwango cha chaji —-hili ndilo pia linasababisha matatizo ya milipuko kwa sasa…endelea kusoma kwa chini tumeelezea zaidi.
Kuishiwa nguvu kwa betri
Betri haiwezi kudumu na nguvu yake kama kawaida; lazima itapungua. Hii inasababishwa na mchanganyiko wa kemikali ambao huwezesha umeme kuzalishwa hivyo na kufanya kuta za Lithium kuwa nyembamba za kusababisha uwezo wa betri kupungua. Kuchaji simu mara kwa mara kupunguza sana ubora wa betri.
Kulipuka kwa betri.
Betri zinazolipuka zinakuwa na nguvu zaidi kuliko uwezo wa Lithium hivyo kama betri zitapewa nguvu zaidi kuliko Lithium lazima zitalipuka. Betri ikipata joto mpaka kufikia nyuzi joto 80Â inakuwa katika hatihati kubwa ya kulipuka.
Pia sababu nyingine kubwa zaidi hasa hasa inayohusiana na milipuko ya simu za Samsung Galaxy Note 7 ni suala zima la kutaka kutengeneza betri nyembamba zaidi kutokana na ushindani wa soko katika uletaji wa simu nyembamba zaidi. Utengenezaji huu wa betri nyembamba sana unasababisha sehemu za betri zisizotakiwa kamwe kugusana – kujikuta zinagusana…na hili linasababisha mlipuko mara moja.
Soma zaidi:
Ni wakati sasa wa kuhakikisha unatumia betri zenye ubora, hakikisha unapotaka kubadilisha betri la simu unanunua kutoka chanzo kinachoaminika.
Na pia weka utamaduni wa kubadilisha betri la simu yako mara moja unapohisi limeanza kutofanya kazi vizuri. – Soma –Â Kubadilisha betri la simu, Ukiona haya ujue muda umefika
Vyanzo: the guardian, mitandao mbalimbali.
One Comment
Comments are closed.