Katika toleo jipya la program endeshaji ya iOs ambalo linajulikana kama iOS 11, limekuja na vipengele vingi vipya ikiwemo na uwezo wa kurekodi sura ya skrini.
Hii inamaanisha unaweza ukawa unafanya vitu vyako katika kifaa chako (iOS) huku ukiwa unarekodi tukio zima linavyofanyika. Kwa mfano unaweza ukawa unaangalia video youtube au hata unachati na mtu huku simu yako ikiwa inarekodi tukio hilo zima,
Watu wengi wamekua wakikumbwa na tatizo la kutoweza kurekodi skrini zao pamoja na sauti (kwa mfano wakiwa wanaongea/ wanakielezea kitu).
Leo Tutakujuza Namna Ambayo Unaweza Kuitumia Kurekodi Skrini Yako Na Pia Video Ikatoka Na Sauti.
Jinsi Ya Kurekodi Video Ya Skrini.
- Kwanza kabisa kama ulikuwa hujawezesha simu yako kuweza kurekodi uso wa simu janja yako, ingia katika Control Center ndani ya ‘Settings’ na kisha nenda katika Customize Controls
- Katika eneo la More Controls ingia katika Screen Recording
- Bonyeza katika kiduara cha kijani chenye alama ya jumlisha kati kati
Sasa baada ya hapo toka katika eneo la Settings na kisha pangusa (Swipe) na kidole kutoka kwenye kingo ya chini ya skrini ya simu yako – kwenda juu ya kingo ya skrini ili kuingia katika ‘Control Center’
Bonyeza kialama cha kurekodi na baada ya sekuunde tatu uso wa skrini yako unaweza ukaanza rekodiwa.
Unawezesha ukasitisha zoezi la kurekodi kwa kubonyeza alama nyekundu ambayo itakua inaonekana juu ya skrini wakati unarekodi au unaweza kuingia tena katika control center na kuweza kusitisha.
lakini ukitumia njia hii ni vigumu kuweza kujua namna ya kuwasha sehemu ya kurekodi na sauti kwani inakua imejizima.
Jinsi Ya Kurekodi Na Sauti
Ili kuwezesha kinasa sauti cha simu janja yako kiweze kurekodi na sauti wakati ukiwa unarekodi uso wa skrini unatakiwa wakati umeingia katika ‘Control Center’ kwa lengo la kurekodi ushikilie kwa alama hiyo ya kurekodi kwa sekunde tatu.
Baada ya hapo yatatokea machaguo na kisha ingia katika ‘Microphone Audio’ na hakikisha kuwa iko On. Mpaka hapo utakuwa umewezesha hili na kuanza kurekodi uso wa skrini ukiwa umeambatana na sauti.
Unaweza ukazuia sauti tena kwa kufuata njia hiyo hiyo uliotumia kuwasha.
Huduma Hii itapatikana kwa watumiaji wa iPhone zenye iOS 11 na kuendelea na vifaa ni Kuanzia iPhone 5S na matoleo ya baada ya hapo.