fbpx

Jinsi ya Kusafisha Kioo cha Laptop au TV

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ushawahi kusikia mtu ameharibu kioo chake cha laptop kwa sababu tuu alikuwa anakisafisha? Kama bado ufahamu uwe inatokea, na sababu kubwa inakuwa ni utumiaji wa njia ambazo si salama kwa vioo (display) vya teknolojia ya LCD.

Hatua ya kwanza:

Zima kifaa chako, iwe laptop au TV yako.

Na kwa usalama zaidi chomoa waya kutoka kwenye umeme kabisa, kwa laptop ikiwezekana chomoa betri – kama imeshindikana hakikisha ulichagua ‘Shutdown’ na wala si ‘Hibernate’ au ‘Sleep’.

Hatua ya pili:

Umeme na unyevu nyevu havipatana, hakikisha umezima kabisa kifaa chako.

Tafuta kitambaa laini na nyororo, ushauri bora kama ukipata vile vitambaa spesheli kwa ajili ya kusafishia miwani basi ndio zitafaa zaidi. Alafu kilainishe kidogo, kumbuka ni kulainisha kiduchu tu….na si kukiloweka kwenye maji. Kitambaa kinatakiwa kisiwe na mimaji maji, maji kidogo ni kwa ajili ya kukifanya kiwe laini zaidi.

kusafisha kioo cha laptop

Tumia maji yaliyochemshwa na kupoa kabisa. Maji yaliyochemshwa yanakuwa salama zaidi kwani hayana madini au chembechembe zinazoweza kuzuru kioo. Kwa ubora zaidi changanya kwa asilimia hamsini hamsini pamoja na Vinegar

INAYOHUSIANA  'IP Address' Ni Nini? Fahamu kuhusu teknolojia hii muhimu

Kwa kitambaa chako safisha kwa juu juu bila kutumia nguvu. Usikandamize kitambaa chako ata kidogo, safisha kwa taratibu na bila kutumia nguvu.

Hatua ya Tatu:

Acha kioo kikauke kwa hewa kwa dadika chache. Kisha tumia kitambaa kikavu na kisafi chenye sifa kama tulizozielezea mwanzoni, pitishia tena taratibu.

Hatua ya Nne:

Subiri dakika zingine 20 – 30, ukiwa na uhakika wa asilimia 100% ya kwamba imekauka kabisa basi chomeka waya na utaweza kuitumia kama kawaida.

Mambo ya Kuzingatia

    • Kamwe usitumie ‘Spray’ ya kusafishia vioo mbalimbali kama vya magari, meza n.k. Hapa naongelea vitu kama vile Windex na za makampuni mengine.
      kusafishia vioo

 

  • Sabuni – iwe ya kuogea, kuvulia n.k, kamwe usitumie maji ya aina yeyote yenye sabuni. Maji ya kulainishia kitambaa chako yanatakiwa yawe masafi sana
INAYOHUSIANA  Tumia Android Au iOS Kama Mouse Katika Kompyuta!

 

 

Je ni njia gani umekuwa ukizitumia? Unadhani ni salama? Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya Teknolojia.

 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Jinsi Ya Kusafisha Kioo Cha Simu Janja! - TeknoKona

Leave A Reply