Kampuni ya Uber yapata Mkurugenzi Mtendaji mpya. Dara Khosrowshashi, mmarekani mwenye asili ya Iran amekuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni ya usafiri ya Uber.
Khosrowshashi ambaye alikuwa mtendaji mkuu wa kampuni ya huduma za usafiri mtandaoni ya Expedia, Jumanne iliyopita alithibitisha kuwa angekubali nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Uber.
Khosrowshashi alitangaza nia yake ya kuchukua uongozi wa kampuni ya usafiri ya Uber yenye makao makuu yake huko San Francisco alipofanya mahojiano na Wall Street Journal na Bloomberg.
Bodi ya wakurugenzi wa Uber walipiga kura Jumapili usiku kumpendekeza Khosrowshashi.
Mwaka huu wa 2017, Uber imehusishwa na kashfa kuhusiana na madai ya watendaji wake kuunga mkono utawala wa Rais Donald Trump na mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia katika makao makuu ya kampuni hiyo.
Ushirikiano wa Uber na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Trump, Travis Kalanick, uliacha kampuni hiyo mwezi Juni katika wakati mgumu.
Lakini Kalanick atabaki kwenye bodi ya Uber na anamiliki kiasi kikubwa cha hisa za kampuni hiyo. Kwa sasa ameshtakiwa na mwanachama mwingine wa bodi ya Uber, Benchmark Capital Partners, ambaye anamshtaki kwa udanganyifu.
Kupitia jarida la Los Angeles Times, Msemaji wa Kalanick ametupilia mbali madai hayo , akisema kuwa mashtaka hayo hayakuwa ya ukweli na yamejaa uongo.