fbpx

Kipengele cha “Private Reply” kiliwekwa kimakosa (kutoka kabla ya muda wake)

1
Sambaza

Makundi kwenye WhasApp yamekuwa na umuhimu wake hasa kwa kuwasogeza watu mbalimbali katika sehemu moja na kuweza kuwasiliana kwa wakati huo huo lakini vipi kuhusu ule uwezo wa kujibu ujumbe kwa njia ya faragha?!

http://coloradomasterstrackandfield.club/author/

http://kseniapphotography.ca/blog/ Inawezekana ulipata bahati ya kuona kipengele fulani kimeongezwa kwenye jumbe za makundi, yaani kuweza kutuma ujumbe wa faragha bila ya mwana kundi mwingine kujua lakini kumbe kipengele hicho kiliachiwa kimakosa (kabla ya muda wake uliokuwa umepangwa kipengele hicho kitoke).

Kipengele cha Reply Private kilitoka katika toleo la majaribio kwenye simu za Windows na baadae kuondolewa baada ya kujulikana kuwa sasisho hilo liliachiwa kimakosa.

WhatsApp Reply Private: Kwenye toleo la 2.17.344 beta kipengele hicho kwenye simu za WIndows hakifanyi kazi tena.

 Facebook ambao ndio wanamiliki WhatsApp wamekiri kuwa sasisho hilo la kuweza kujibu jumbe kwa njia ya faragha haikuwa sahihi kutoka kwa wakati ule. Kipengele cha kuweza kutuma/kujibu ujumbe wa faragha unaweza kunakilika na kuweza kutumwa kwa mwingine kwa njia ya wazi (personal chat).

Kipengele cha kutuma ujumbe wa aina fulani ambao hutaki mtu mwingine ajue kama umetuma ulikuwa na kasoro fulani fulani kama vile kipengele hicho kipya kuonekana kwenye mazungumzo ya kawaida badala ya kwenye makundi ya kwenye WhatsApp tu.

Kipengele cha “Private Reply” kinatarajiwa kutoka pamoja na masasisho mengine kama uwezo wa kubadilisha mazungumzo ya kwa njia ya sauti na kwenda kwenye mazungummzo ya video bila kuathiri mazungumzo hayo.

Vyanzo: WebInfo, Gadgets 360, The Indian Express

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu mbili za Samsung kupata Android 9 Pie Januari 2019
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|