fbpx

Kompyuta/Tabiti isiyochosha kuibeba

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika miaka kadhaa sasa makampuni mengi yamejaribu kutoka kompyuta mpakato ambazo zinaweza kutumika katika namna mbili tofauti; kutumia kama kompyuta au tabiti katika kifaa hicho hicho.

Smartron T-Book Flex ndio kompyuta/tabiti ambayo imetoka baada ya miaka miwili kupita tangu mtangulizi wake. Ni kifaa ambacho huwezi kuhisi karaha kutembea nacho kwani sio kizito kabisa na kumfanya mtu asiweze kufurahia pindi anapokuwa amekiweka kwenye mfuko.

Mchanganuo wa sifa za Smartron T-Book Flex.

Keyboard

Kwa mtu yeyote anayependa kutumia kompyuta mara kwa mara kwa shughuli zinazzohusiana na kuandika basi atapenda kuwa na kompyuta amabyo ina keyboard yenye vitufe vya kubonyeza imara na ndivyo ilivyo kwenye kompyuta/tabiti, Smartron T-Book Flex.

isiyochosha kuibeba

Keyboard ya hii inaweza kutenganishwa na kutumia hata kama haijaunganishwa na kompyuta kwa kutumia bluetooth. Vilevile inaweza kutumiwa hata sehemu ambayo kuna mwanga hafifu na mtumiaji asipate tabu ya kujua kitufe cha kubonyeza.

Tabiti

Umuhimu wa tabiti unaonekana pale ambapo unahitaji kifaa chako kwa matumizi ya kawaida sana na pengine unataka kutembea na kifaa hicho kwa urahisi zaidi.

isiyochosha kuibeba

Smartron T-book Flex kama tabiti inafanya kazi kazi kwa ufanisi, kasi nzuri na hata upande wa teknolojia ya mguso hauna shida ya kukwamakwama wakati mtu anaitumia.

Sifa

Uwezo

 Prosesa Zipo katika toleo mbili tofauti; Kizazi cha saba cha Intel Core m3 na Core i5. Kasi ya prosesa ni 2.4GHz na 5GHz mtawaliwa.
Kioo Kina ukubwa wa inchi 12.2, ubora wa picha: 2560×1600 pixels. Ina kalama maalum pia kioo kinaweza kuzunguka mpaka nyuzi 150.
Diski uhifadhi/RAM Ina GB 128 SSD pia unaweza kuweka memori kadi kadi.
Betri Betri yake ni Lithium-ion Polymer yenye 40Whr.
Kamera Ina kamera mbaili; kamera ya mbele ina MP 2 na ile ya nyuma ina MP 5.
Programu endeshi Inatumia Windows 10.
Bei

Core m3 ni $637| Tsh. 1,433,250 na Core i5 $ ni 786| Tsh. 1768,500

Usalama Ina teknolojia ya fingerprint
Wembamba Ukubwa wa tabiti: 307.5 x 202.8 x 9.0 mm uzito wake ni gramu 950 bila keyboard na Kg 1.3 ikiwa na keyboard
Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni Ina ukubwa wa 3.5mm
Rangi Machungwa, Kahawia, Nyeusi-Kahawia
Teknolojia nyinginezo  Ina USB 3.0, USB Type C Thunderbolt 3 kwa ajili ya sehemu ya kuchaji, sehemu ya ziada kuchomeka keyboard ya nje, Wi-Fi Direct, and Bluetooth 4.0.

 

INAYOHUSIANA  Chrome 74: Jinsi ya kuweka muonekano wa giza kwenye simu/kompyuta

Kompyuta/tabiti, Smartron T-Book ndio hiyo sasa wewe kama mdau wa teknolojia kifaa hiki kimekuvutia na pengine hata ukaamua kukinunua?

Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|