Uko tayari kwa kongamano la pili la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano? Taarifa ni kwamba kongamano hilo linafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kongamano la mara ya kwanza lilifanika Okt 26-27 2017 na kwa ujumla mengi yalizungumzumzwa na wataalam katika masuala ya teknolojia na TEHAMA kwa ujumla wake. Tujikumbushe kidogo kongamano lililopita lilihusisha mambo gani bofya hapa.
Kama kawaida jukumu la kamisheni ya TEHAMA ya Tanzania (ambao ndio waandaaji wa kongamano hilo) ni:-
- Kusaidia na kukuza uwekezaji katika TEHAMA Tanzania,
- Kukuza na kuendeleza taaluma na kiwango cha TEHEMA,
- Kushauri na kushirikiana na washikadau mbalimbali katika utafiti, upangaji wa viwango na katika swala zima la mitizamo,
- Kuendeleza miundombinu na programu mbalambali zinazohisiana na TEHAMA ikiwemo na kuendesha zoezi zima.