fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Intaneti Maujanja whatsapp

Sio ndani dakika 7 tu! Unaweza kufuta ujumbe hata baada ya siku 7 katika WhatsApp #Maujanja

Sio ndani dakika 7 tu! Unaweza kufuta ujumbe hata baada ya siku 7 katika WhatsApp #Maujanja

Spread the love

Siku chache zilizopita tuliandika kuhusu uwezeshwaji wa uwezekano wa kufuta ujumbe uliotumwa kwa mtu au kundi kupitia programu ya WhatsApp.

Katika makala hayo uwezekano wa kufuta ujumbe uliokwisha tumwa ni ndani ya dakika saba tu na si vinginevyo. Ni kwamba baada ya kupita kwa muda huo hutaweza kuwa na uwezo wa kufua ujumbe huo kule ulipokwenda.

Lakini leo kupitia hapa TeknoKona tutakuelekeza kufuta ujumbe ulioutuma kwa mtu au kundi katika WhatsApp zaidi ya muda huo uliowekwa rasmi na WhatsApp wenyewe. Cha kwanza ni kuangalia ujumbe unaotaka kuufuta je uliutuma lini. Angalia tarehe ya siku uliyotuma ujumbe huo.

Kwa muhtasari, utaratibu ni kama ifuatavyo:

1. Funga Data katika simu yako (Wifi na data)
2. Usifungue programu ya WhatsApp
3. Badilisha tarehe ya simu yako (siku kabla ya ujumbe)
4. Fungua Whatsapp yako
5. Chagua ujumbe unaotaka kufuta, futa.
6. Rekebisha tarehe ya simu yako (Hiari)
7. Washa data
8. Baada ya kuwasha data ujumbe kule ulikoutuma utafutika.

Namna ya kufuta Ujumbe uliopita muda wa Dakika 7.

>Kwanza kabisa funga programu yako ya WhatsApp. Kisha zima Data katika simu yako. Yaani simu isiwe imeunganishwa na intaneti kwa namna yoyote. Kama unatumia Wi-Fi kupata intaneti pia zima.

SOMA PIA  Spotify kupatikana Tanzania, ni habari njema kwa wapenda muziki

>Nenda wenda kwenye mpangilio (Setting) wa simu yako kubadilisha tarehe au saa. Weka tarehe ya siku uliyotuma ujumbe huo kisha nenda kafungue WhatsApp yako. Na uingie katika ukurasa wenye ujumbe uliokusudia kuufuta. Ubonyeze ujumbe huo kisha uufute.

kufuta ujumbe hata baada ya siku 7 katika whatsapp

kufuta ujumbe hata baada ya siku 7 katika whatsapp: Namna ya kurekebisha tarehe au saa katika simu yako. Namba 2 ondoa hiyo tiki ili uweze kurekebisha tarehe au saa

Je, ujumbe ambao bado ni siku hiyo hiyo lakini muda wa dakika saba umepita unafanyaje? Utaratibu hauna tofauti sana na huo mwingine. Unachotakiwa ni kujua ni saa ngapi uliutuma ujumbe huo. Mfano umetuma ujumbe saa saba kamili mchana, unachotakiwa ni kurudisha saa ya simu yako kuwa saa sita na dakika yoyote upendayo. Iwe kamili au na dakika kadhaa ni wewe tu.

Hatua za kufuta ni zile zile ni kuubonyeza ujumbe unaokusudia kuufuta na kisha utabonyeza kitufe cha alama ya delete ambacho kipo juu. Na kisha itatokea menu yenye meseji tatu. Moja inasema DELETE FOR ME, CANCEL na DELETE FOR EVERYONE.

Ili ufute ujumbe kule ilipokwenda inabidi ubonyeze DELETE FOR EVERYONE. Baada ya hatua hiyo washa Data katika simu yako na ujumbe kule ulipokwenda utajifuta kama kawaida ya utaratibu wa ndani ya dakika Saba.

Zoezi hili tumelifanyia kazi na tumelithibitisha linawezekana bila ya tabu yoyote. Bila shaka maujanja haya yatakuwa yamekusaidia. Jaribu na wewe uone maujanja haya. Usisitize kutupa maoni yako hapo chini.

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania