fbpx

Njia rahisi ya kutunza au kutafuta ukurasa uliouhifadhi kwenye kivinjari

0

Sambaza

Kusoma vitu kwenye mtandao kwa kutumia kompyuta ni kitu cha kawaida sana na kuna wakati unataka uweze kuutunza ukurasa fulani wenye habari ambayo unataka kuja kuisoma baadae lakini inakuwa changamoto kidogo kwako.

Unaweza ukafikia uwamuzi wa kutafuta mtaalam wa masuala ya kompyuta au mtu ambae ni mtundu mtundu kwenye kompyuta ili akusaidie kuutunza ukurasa wa kwenye tovuti fulani kwenye kivinajri. Huhitaji msaada wa mtu yeyote isipokuwa wewe mwenyewe tu!

Namna ya kutunza ukurasa kwenye kivinjari.

Kama wewe unatumia kivinjari mara kwa mara (iwe kwenye simu/kompyuta) utakuwa go to link umeshaona alama ya nyota/kopa upande wa kulia kabisa kwenye uwanja wa kuandika tovuti. Basi leo fahamu ya kuwa ukibonyeza kitufe hicho (alama ya nyota/kopa) utakuwa umeuhifadhi ule ukurasa bila kunakili jina la tovuti kwa ajili ya wewe kukumbuka hapo baadae.

ukurasa uliouhifadhi

Unaweza ukabonyeza alama ya nyota au ukatumia njia fupi (bofya CTRL+D kwenye kicharazio cha kompyuta) kuweza kuhifadhi ukurasa na kuupa jina utakalopenda ili uweze kukumbuka kirahisi.

Jinsi ya kutafuta ukurasa uliouhifadhi.

Inawezekana umetunza lakini sasa hujui namna ya kuupata ule ukurasa ambao uliutunza wakati fulani kwa lengo la kutaka kuutembelea wakati wowote utakapohitaji na njia rahisi na kamwe haitakusumbua ni kubonyeza  http://local-ice.com/?> CTRL+SHIFT+B (kwenye Windows) au  get link Alt + ⌘ (kwenye kompyuta za MAC).

ukurasa uliouhifadhi

Huu ndio ukurasa ambao utaona tovuti zote ambazo ulizifidhi kwenye kivinjari husika.

Kwa wanaotumia kompyuta za MAC inaweza kuwa rahisi zaidi kupata kurasa walizozihifadhi.

ukurasa uliouhifadhi

Njia nyingine rahisi ya kuona tovuti ulizozihifadhi kupitia hapohapo kwenye kivinjari.

Hii inamaanisha hakutakuwa na haja tena ya kufungua kurasa nyingi kwenye kivinjari kisha kutozifunga baada ya kumaliza kusoma/kufanya kitu kingine kwa hofu ya kuupoteza ukurasa husika.

Vyanzo: Opera Blogs, Mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uwekezaji katika sarafu ya za kidijitali nchini Tanzania
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.