fbpx

Lijue Kongamano La ‘Annual ICT Professionals Conference’ – AIPC 2018! #Tanzania

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tume ya TEHAMA ya Tanzania imeandaa kongamano la pili ambalo linajulikana kama “Annual ICT Professionals Conference 2018” ikiwa ni moja kati ya juhudi zake  katika kukuza tehema tanzania.

AIPC ni moja kati ya majukwaa muhimu sana kwa wana TEHAMA wote kwani ni sehemu ambayo unaweza ukapata mambo kede kede ikiwemo kama vile kujua jinsi maswala ya TEHAMA yanavyokwenda duniani, kutengeneza mahusiano na watu mbalimbali katika kongamano hata kuonyesha bidhaa zako (kama unazo) n.k.

Ijulikane kwamba kongamano hilo kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka jana katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu nyerere, japo na mwaka huu litafanyika huko huko mambo mengi makubwa yanategemewa kutoka katika kongamano hili.

INAYOHUSIANA  Watumishi wa serikali kutumia TTCL sasa ni lazima!

Kongamano linaweza hudhuriwa na mtu yeyote lakini inapidi alipie ushiriki wake, hivyo kwa maelezo zaidi juu ya kujiandikisha unaweza kutembelea: www.ictc.go.tz : au barua pepe: info@ictc.go.tz

Ikumbukwe kwamba kongamano hili linaweza kuhudhuriwa kwa kujiandikisha tuu na si vinginevyo. TeknoKona ni moja kati ya mbia/mshirika katika AIPC 2018.

Picha ya pamoja katika kongamano la wanateknolojia (AIPC) mwaka 2017. TeknoKona iliwakilishwa na watu wawili, mmoja kati yao ni mtu wa pili kutoka kushoto.

Kongamano litakua ni la siku tatu na litaanza tarehe 24 mpaka 26 mwezi Oktoba 2018. Mada mbalimbali zitazungumzwa ikiwemo na maudhui ya nyumbani kuhusiana na TEHAMA, ubunifu na ujasiliriamali. Ukuaji wa viwanda na hata ulinzi na usalama haswa ule wa mtandaoni.

INAYOHUSIANA  Podcast ni nini? - Njia rahisi ya kusikiliza na kurusha vipindi kwa urahisi

Mambo kama changamoto za kuanzisha kitu (Biashara) katika TEHAMA tanzania yatazungumzwa, pia kutakuwa na maonyesho kutoka kwa wawekezaji na pia hata uwekezaji utakuwepo katika nyanya mbali mbali za TEHAMA.

TeknoKona ikiwa kama mmoja kati ya wadau wa kongamano hili itakua mara kwa mara inakupa taarifa fupi juu ya mambo yaliyotokea .Ili kuhudhuria kongamano hili basi huna budi kuwasiliana na tume ya TEHAMA na kufuata taaratibu zote za kujiandikisha.

Endelea kutembelea TeknoKona kila siku ili kujipatia yote yanayojiri katika teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.