fbpx

Mapya kutoka Apple: iPad Pro 2018 na Penseli Janja

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Apple wametambulisha bidhaa kadhaa mwisho wa mwezi Oktoba 2018. Katika tukio lililofanyika tarehe 30 huko nchini Marekani Apple walitambulisha MacBook Air 2018, Mac Mini, iPad Pro 2018 pamoja na Penseli janja kwa ajili ya kutumika katika iPad Pro.

Unaweza kusoma uchambuzi wa MacBook Air 2018 na Mac Mini – HAPA.

Katika makala hii tutazungumzia iPad Pro 2018 pamoja na penseli janja inayokuja nayo.

iPad Pro 2018

Kwa kiasi kikubwa tableti ya iPad inazidi kupewa nguvu ya kutumika kama kompyuta kamili. iPad Pro mpya kutoka Apple ina ukubwa wa inchi 11, huku ikiwa na display ya HD kubwa ikitumia display ya LCD iliyopewa jina la Liquid Retina.

iPad Pro 2018

iPad Pro 2018: Muonekano wa iPad Pro

Apple wamesema iPad Pro hiyo ina kasi ya karibia mara mbili zaidi ukilinganisha na toleo lililopita, na pia uwezo wake wa ki’graphics (yaani kwa app za ubunifu na magemu) ni mara 1,000 zaidi bora ukilinganisha na toleo lililopita.

INAYOHUSIANA  Apple kuzibania apps za Facebook na WhatsApp kwenye iPhone

Mengineyo
– Inakuja na teknolojia ya Face ID ili kuweza kutambua sura na kuondoa kufunguka.
– Home button imeondolewa ili kuzidi kuwa na nafasi kubwa kwa ajili ya display.
– Kuna matoleo mawili, toleo la inchi 11 na inchi 12.9.
– App ya Photoshop yenye uwezo mkubwa kama wa kwenye kompyuta inaweza fanya kazi kwa ufanisi mzuri tuu.
– Bei: Bei inaanzia dola 799 (Takribani Tsh 1,800,000/=) kwa toleo la inchi 11, na dola 999 (Takribani Tsh 2,300,000/=) kwa toleo la inchi 12.9

Apple Pencil

Penseli janja hii kutoka Apple inalenga kutumika na iPad Pro. Inakuja na uwezo wa kunasa kwenye eneo la juu la iPad Pro kwa sumaku, na ikishanasa inauwezo wa kupokea chaji ya umeme kutoka kwenye iPad Pro moja kwa moja bila uhitaji wa waya wowote.

ipad pro 2018 pencil

Penseli ikiwa imenasa juu ya iPad Pro 2018.

Vitu vyote hivi vimetengenezwa kwa kutumia malighafi zilizokwishatumika (Recycle)

  • MacBook Air, iPad Pro na Mac Mini vyote vimetengenezwa kwa kutumia malighafi zilizokwishatumika za alumini (Aluminium).
  • Apple wamesema wameweza kutumia timu yao ya wahandisi kufanikisha utengenezaji wa bidhaa zao hizi mpya kutumia malighafi za alumini zilizokwishatumika kwa asilimia 100.

Je una mtazamo gani juu ya iPad Pro hii?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.