fbpx
Teknolojia

Mboga ya majani aina ya ‘Spinach’ kutumika kugundua bomu

mboga-ya-majani-aina-ya-spinach-kutumika-kugundua-bomu

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Inawezekana ulijua tu mboga tunakula hutusaidia kujenga mwili na kutukinga dhidi ya maradhi lakini mboga za majani aina za ‘Spinach’ zinauwezo wa kipekee zaidi kwani zinaweza zikatumika kugundua mabomu.

Wanasayansi wameweza kuifanya mboga ya aina ya Mchicha au ‘Spinach’ kugundua bomu. Katika utafiti uliofanywa na wanasayansi wa MIT wamegundua kwamba … majani ya mchicha yanaweza kuhifadhi kemikali aina ya ‘Nitro-aromatics’ ambazo hupatikana kwenye mabomu ya kutegwa arthini na silaha zinazozikwa ardhini

INAYOHUSIANA  Kondom Itakayoweza Kuua Vijidudu na Kutopunguza Raha ya Tendo

Si lazima mboga hii iwekwe nyaya yoyote ili kuweza kugundua bomu bali vikompyuta vidogo ‘nanocomputers’ zinazowekwa kwenye mmea huo vitaweza kupata taarifa kama kuna madini yaliyonyonywa kupitia mizizi yake na kuyatambua kama ni ya bomu..kisha taarifa itatumwa kwenda kwenye kifaa kama simu au kompyuta ya mtu kwa kutumia mfumo wa WiFi au Bluetooth.

Mboga ya majani aina ya Soinach inafanyiwa uchuzi zaidi kuweza kujua mengineyo.
Mboga ya majani aina ya Soinach inafanyiwa uchuzi zaidi kuweza kujua mengineyo.

Jinsi utafiti huo ulivyofanyika

Wanasayansi waliweka kemikali za Carboni kwenye maji na kisha kufanya mizizi ya mboga kupitisha maji yale hadi kwenye matawi ya mchicha. Kisha wanasayansi wakapapasa majani ya mchicha kwa kutumia vyuma maalum na majani yale yalianza kutoa chembechembe za moto ambazo zinaweza kuonekana kwa kompyuta.

INAYOHUSIANA  Kompyuta/Tabiti isiyochosha kuibeba
Kwa ugunduzi huu matumizi ya mbwa, panya yatapungua kwa kiasi kikubwa utafiti huu ukienea duniani kote.
Kwa ugunduzi huu matumizi ya mbwa, panya yatapungua kwa kiasi kikubwa utafiti huu ukienea duniani kote.

Pia chembechembe hizo zinaweza kuonekana kwa simu ya mkononi. Wanasayansi  wanasema mboga ya mchicha pia inaweza kutumika kufahamu uwepo wa visima vya maji ardhini, kemikali zilizovuja kutoka kwa silaha na madini ya Nitro-aromatics.

Kwa sasa wanasayansi wananuia kuwezesha mboga hiyo kuweza kugundua bomu lililotegwa umbali mrefu ardhini. Tuambie mtazamo wako kuhusiana na hili.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Chanzo: BBC na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|