fbpx

Mlipuko wa simu wamuua msichana wa miaka 18

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Msichana mwenye umri wa miaka 18 nchini India aitwaye Uma Omram amefariki dunia kwa mlipuko uliosababishwa na simu ya Nokia 5233 wakati alipokuwa anaitumia kuongea.

Taarifa zinasema binti huyo alikuwa anaongea na simu hiyo iliyokuwa imechomekwa kwenye chaji ndipo mlipuko huo ulipotokea. Mlipuko huo ulimjeruhi mkono wake, mguu na kifua na baadae alikimbizwa hospitalini ambako ilithibitishwa kuwa ameshafariki.

mlipuko wa simu

Simu ya Nokia-5233 iliyolipuka; Nokia 5233 ilizinduliwa Januari 2010 na bado inauzwa kupitia mtandao wa Amazon wa India kwa Rupia 2,999 sawa na Shilingi za kitanzania 104,053.

Wakizungumzia tukio hilo kampuni ya HMD Global ambao ndio wazalishaji wa simu za Nokia walisema hawahusiki na simu hiyo kwa kuwa sio wazalishaji kwa kipindi simu hiyo inatolewa.

Kampuni ya HMD Global ilinunua jina la Nokia kuanzia Desemba 2016 na haijulikani nani atawajibika kwa tukio la binti huyo. Wamiliki wa Nokia wanasema ingawa hawawezi kuthibitisha tukio hilo lakini pia wanadai hawawajibiki kutokana na tukio hilo kwani simu hiyo haikuuzwa chini ya kampuni yao.mlipuko wa simu

Matukio ya simu kulipuka sio mara ya kwanza kutokea kwani Samsung nao walishawahi kukumbwa na kashfa ya moja ya simu zao kulipuka jambo lililowaweka katika wakati mgumu kibiashara. Lazima tukubali kuwa ni hatari sana kuongea na simu wakati inachajiwa.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  BlackBerry Messenger (BBM) kufungwa Mei 31
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.