Kwa muda tuu zimekuwepo habari zikihusisha mpango wa Google kutaka kurudi Uchina jambo amabalo limezua wasiwasi kwa wanasiasa nchini Marekani na kutaka kupewa maelezo ya kina.
Dunia nzima inafahamu ukiwa nchini Uchina huwezi kupata huduma ya Google na hii ni baada ya Google kuacha shughuli zake mwaka 2010 lakini huenda mambo yakarejea kama hapo awali.
Wanasiasa takribani kuna na wa sita (16) kutoka vyama vya Republicans na Democrats wameiandikia barua Google wakiitaka kueleza kama wanayoyasikia yana ukweli wowote au la!
Kinachotia hofu zaidi ni kwamba Google wanatengeneza toleo la ambalo litazua tovuti zinazozunguzia demokrasia, dini, haki za binadamu na maandamano huko Uchina.
Moja ya viongozi wa juu kutoka Google amedai kuwa hawana mpango wa kupeleka kitu kinachodaiwa nchini Uchina katika siku za usoni. Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wamediriki kuacha kazi kama ishara ya kutokubaliana na mpango huo.
Baidu ndio mbadala wa Google nchini Uchina kwa sasa na iwapo kama kinachosemwa kikatimia basi wananchi nchini Uchina watakuwa kwenye kifungo cha aina yake.
Vyanzo: Engadget, Reuters