fbpx

Mswada wa matumizi ya simu kwa watoto

0
Sambaza

Wabunge nchini Ufaransa wamepitisha mswada wa sheria ambao utapiga marufuku matumizi ya simu rununu  na tabiti katika shule za nchini humo hususani katika muda wa masomo.

can you buy viagra off the counter

orlistat diet pill mexico Kwa mujibu wa mswada huo wanafunzi wa umri wa chini ya miaka 15 hawataruhusiwa kuwa na simu wala tabiti katika maeneo ya ndani ya shule au wazizime iwapo watakuwa nazo.

Viongozi ambao wanaunga mkono mswada huo wamesema sheria mpya itasaidia kuzuia ongezeko la simu mashuleni na kupunguza upotevu wa muda kwa wanafunzi kutazama picha badala ya kusoma na kujifunza masomo ya shuleni.

mswada

Matumizi ya simu mashuleni kwa ughaibuni: Takwimu zikithibitisha watoto wanaosoma shule za serikali wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii.

Kawaida wanafunzi nchini Ufaransa waliruhusiwa kuwa na simu shuleni lakini hawakuruhusiwa kuzitumia wakiwa darasani kitu ambacho wanafunzi wengi hawakuzingatia na badala yake walizitumia ndani ya madarasa yao.

Sambamba na sheria hiyo pia kumekuwa na mapendekezo katika sehemu za kazi itungwe na sheria kama hiyo ili kudhibiti wafanyakazi wanaotumia muda mwingi kuchezea simu zao kwa kuperuzi mitandao ya kijamii na kutumiana ujumbe mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Motorola RAZR ipo njiani kuja lakini kivingine
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.