fbpx

Mwanasayansi agundua Viwavi jeshi wanaokula Plastiki na kuozesha ndani ya wiki

0
Sambaza

Kwa wastani kila mfuko wa plastiki unatumiwa na binadamu kwa nusu saa tu, lakini unahitaji mamia ya miaka kuoza katika mazingira ya kimaumbile.

enter site Kwa sababu mfuko huo unazalishwa kwa kemikali ya Polyethylene, ambayo ina muundo imara na ni vigumu sana kuoza. Hivyo suala la kushughulikia takataka za plastiki limekuwa tatizo linalowasumbua wanasayansi kwa muda mrefu.

watch Pamoja na hali hizo kuna matumaini ya kupatikana ufumbuzi wa kero za takataka zinazotokana na mifuko ya Plastiki.

viwavi jeshi wanaokula plastiki

Viwavi jeshi wanaokula plastiki: Viwavi jeshi hawa watakuwa ni jibu nzuri kwa vita dhidi ya uharibifu wa mazingira unaosababishwa na mifuko ya rambo

Mwanasayansi wa Italia huenda akawa amegundua njia mpya ya kutatua tatizo la takataka za plastiki. Aina moja ya wadudu wanaweza kubadilisha plastiki kuwa kemikali ya Ethylene Glycol kwa kuila. Utafiti huo umetolewa hivi karibuni kwenye gazeti la Current Biology.

INAYOHUSIANA  Miaka 25 ijayo huenda mwanadamu akatua Sayari ya Mars

Bw. Federica Bertocchini kutoka Italia aliona kwa bahati kuwa mfuga nyuki mmoja aliwakamata wadudu kadhaa wanaokula nta kwenye mzinga wa nyuki, na kuwaweka ndani ya mfuko wa plastiki. Lakini dakika chache tu wadudu hao walikula baadhi ya plastiki na kutoroka.

Mwanasayansi agundua wadudu wanaokula Plastiki : Bibi Federica akionesha mmoja wa wadudu hao kwenye kidole chake

Baadae mtafiti huyu aligundua kuwa wadudu hao wadogo wa nondo aina ya Pyralidae si kama tu wanakula plastiki, bali pia wanaimeng’enya na kuibadilisha kuwa kemikali ya Ethylene Glycol.

Kemikali ya Ethylene Glycol inaweza kuoza udongoni au majini ndani ya wiki chache tu tofauti na Polyethylene, .

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.