Ndio, ndio kwa kishindo kabisa kampuni ya Nokia imerudi tena na sasa simu janja zake zinaendeshwa na programu endeshi ya Android.
Ujio huu wa Nokia uliwafurahisha wengi kwani ukizingatia Nokia ndio lilikua kampuni ambalo limeteka soko la simu duniani miaka kadhaa iliyopita. Kampuni limeshatoa simu nyingi tangia lirudi katika soko la simu.
Hivi sasa wameingia mkataba wa kushirikiana na kampuni inayojulikana kama Zeiss. Zeiss ni maarufu kwa kutengeneza Lenzi za kamera na kwa haraka haraka ni kwamba Nokia inaweza ikatoa simu zenye kamera kutoka kampuni hilo
Kingine ni kwamba kama hujui hii sio mara ya kwanza kwa kampuni kuingia katika mkataba na kampuni hiyo (Zeiss) kwani hata hapo awali hili lilifanyika na ikatoka simu ya Nokia yenye Lenzi kutoka katika kampuni la Zeiss.
Mpango wa kampuni kwa sasa ni kuleta simu janja ya maana kulinganisha na zile ambazo wamezitoa (Mfano Nokia 6 ambayo inaingia sokoni mwezi julai 2017) ambayo itakua na ushindani mkubwa kulinganisha na simu ambazo zimeliteka soko kwa sasa.
Ni wazi kwamba uwezo wa kamera katika dunia ya sasa ni kitu moja wapo ambacho kinaipa simu janja sifa za juu — hilo kmpuni imeliona — kabisa.
Jambo hili pengine limefanyika baada ya kampuni ya Nokia kupoteza wataalamu wengi ambao waliondoka baada ya kampuni kumilikiwa kwa muda na Microsoft, Hivyo inawalazimu tuu kuingia mkataba na Carl Zeiss.