Ripoti TCRA: Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Kufikia milioni 23

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya mpaka Desemba 2017 imeonyesha kuwa idadi ya watumiaji wa intaneti imeongezeka kufikia watu milioni 23 ambayo ni sawa na asilimia 45 ya Watanzania wote.

Takwimu imeonesha kuna ongezeko kubwa la watumiaji wa Intaneti mwaka hadi mwaka.

Takwimu ya mwaka 2012 ya watumiaji wa Intaneti ilikuwa ni milioni 7.52 ambayo ni asilimia 17 wakati mwaka 2013 wakaongezeka kufikia milioni 9.31 sawa na asilimia 21.

Idadi ya watumiaji wa Intaneti

Takwimu za watu wenye laini za simu

Mwaka 2014 watumiaji walifikia milioni 12.17 sawa na asilimia 29, mwaka 2015 watumiaji waliongezeka kufikia milioni 17.62 sawa na asilimia 34 na mwaka 2016 idadi ilifika milioni 19.86 sawa na asilimia 40.

Je neno ‘watumiaji’ ni neno sahihi? Tukumbuke ni kawaida mtu kumiliki vifaa vingi vya intaneti.

Data zinaonesha watumiaji wa mitandao ya kijamii kama Instagram na hata Facebook bado ata milioni 10 hawajafikia kwa Tanzania.

Ripoti hiyo pia inaonesha kuwa idadi ya watumiaji wa simu za mkononi imefikia milioni 40 kutoka milioni 27.62 mwaka 2012, huku mtandao wa Vodacom ukiongoza kwa kuwa na watumiaji waliojisajili 12,714,297 wakifuatiwa na Tigo kwa kuwa na watumiaji waliosajiliwa 11,062,852.

INAYOHUSIANA  Uwezo wa Kupiga Simu WhatsApp Waanza Kusambaa

Katika aina ya Intaneti inayotumika na watu wengi zaidi ni ile inayohamishika yaani ‘wireless’ ina watumiaji wapatao milioni 19 na milioni 3.4 intaneti isiyohamishika na wale wa wanaotumia wired idadi yao ni  520,698.

Je una mtazamo gani juu ya idadi hii? Kwa Teknokona tunaona kuna umuhimu wa TCRA kuanza kutafiti jina jingine la data za ‘subscriptions’ na kuacha kuitumia kama idadi ya watumiaji.

Kwa kiasi kikubwa data zitakuwa zinapokelewa vingine kwani ni kawaida watu wengi watumiaji intaneti kuwa na simu mbili au hata zaidi. Na kama simu zote hizo zinazotumia intaneti zitahesabiwa kama ni watu tofauti basi idadi hii itaendelea kupaa na labda ata kufikia asilimia 100 au zaidi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.