Inaonekana zoezi la kufungua simu ambazo sio halisi halikufikia tamati kwani idadi mpya imetolewa ambapo rungu la TCRA limezifika simu zaidi ya nne elfu.
Miaka kadhaa imepita tangu mamlaka ya mwasiliano Tanzania (TCRA) kufungia simu ambazo zilibanikika kutokuwa halisi na kwa kiasi fulani kuna watu waliathirika kutokana na zoezi hilo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mamlaka hiyo hivi karibuni imebainisha kufungua simu 4,340 baada ya kubainika kuwa na walakini wa kutokuwa halisi, kuibiwa (simu ya wizi) au kununuliwa kwenye maduka yasiyo rasmi lakini pia zikiwa chini ya kiwango.