fbpx
simu, Teknolojia

Samsung Galaxy S8: Samsung watengeneza simu rahisi zaidi kuvunjika kisha waitengenezea kikava

samsung-galaxy-s8-simu-rahisi-zaidi-kuvunjika

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Simu ya Samsung Galaxy S8 baada ya kupitia majaribio kadhaa imeonekana ndio simu ambayo ni rahisi zaidi kuvunjika kuliko simu zingine zozote kwa sasa.

Kutokana na aina ya ubunifu wa kioo/display kwenye simu za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus kumeifanya simu hizo kuwa rahisi zaidi kuvunjika kuliko simu zingine zozote.

‘Simu moja ya Galaxy S8/S8 Plus ikianguka mara moja tuu chini ina asilimia kubwa zaidi kuvunjika kioo chake vibaya ukilinganisha na simu zingine’

simu rahisi zaidi kuvunjika samsung galaxy s8
Simu rahisi zaidi kuvunjika: Muonekano wa Galaxy S8 baada ya kuanguka na kuvunjika
Muonekano wa Galaxy S8 – Inakuja na toleo la Android Android 7.0

Utafiti ulijumuisha simu hizo kuangushwa kutoka urefu wa futi 6 na kuangukia kwenye eneo la sakafu. Kampuni moja wapo, SquareTrade, ambayo huwa inafanya tafiti za namna hii kwa simu za aina mbalimbali imesema simu za S8 ndio simu za kwanza kwenye utafiti wao kuvunjika maeneo mengi zaidi kwa kuanguka mara moja tuu.

INAYOHUSIANA  Vaio Waja Na Simu Janja Yenye Mfumo Wa Android!

Habari nzuri?

Habari nzuri ni kwamba Samsung wamehakikisha vipuri (spare) za simu hizi zitakuwa bei rahisi zaidi ukilinganisha na matoleo ya simu za familio hiyo zilizopita – screen/kioo chake kitakuwa bei nafuu zaidi kwa tofauti ya bei ya kati ya tsh 100,000 hadi 200,000 ukilinganisha na cha Galaxy S7.

Pia Samsung wamekuja na vijikava vidogo kwa ajili ya kuvalisha simu hizo. Ukivalisha kikava hichi basi athari ya kuanguka na kuharibiba vibaya inapungua zaidi ukilinganisha na kama ikianguka bila kava hii.

INAYOHUSIANA  Samsung: Jinsi itakavyokuwa simu ya mkunjo
Simu ya Galaxy S8
Simu ya Samsung Galaxy S8 ikiwa imevalishwa kijikava kimpya kinachokuja kikiwa vipisi viwili, kimoja kinapachikwa chini na kingine juu.

Kava hizi zitauzwa kwa takribani Tsh 40,000/= na zitaweza tumika kwenye simu za aina zote za S8.

Ulipitwa na uchambuzi wa simu ya Samsung Galaxy S8 na S8 Plus? Soma hapa – Uchambuzi, Samsung Galaxy S8 na S8 Plus

Chanzo: Mitandao

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |