fbpx

Samsung kuondoa ‘Earphone Jack’

0
Sambaza

Ripoti mpya zaidi kutoka vyombo vya habari vya Korea Kusini vinasema huenda Kampuni ya Samsung ikaondoa sehemu ya kuchomekea spika za masikioni (earphone jack) katika simu zake za matoleo yajayo.

order diflucan from canada

Taarifa hizo zinasema huenda Samsung Galaxy Note 10 ikawa ndio simu ya kwanza kutoka kampuni hiyo kutokuwa na sehemu hiyo.  follow url Hakuna sababu zilizotajwa kwanini Samsung inachukua hatua ya kuondoa kitu hicho kwenye simu zake, lakini ripoti inasema kwa familia ya simu za ‘S’ inaweza kusubiri mpaka kufikia toleo la Samsung S11.

Earphone/Headphone jack ni ile sehemu yenye tundu la kuingizia spika za masikioni kwa ajili ya kusikilizia muziki masikioni au kuchomeka Spika kwa usikivu mkubwa zaidi.

Earphone Jack

Kuondolewa kwa sehemu ya kuchomekea spika za masikioni kutasababisha nafasi yake kuchukuliwa na USB Type-C.

Taarifa hii ya kuondolewa kwa sehemu ya kuchomeka spika za masikionu kwa matoleo yajayo ya Samsung imepokewa kwa namna tofauti na wapenzi wa simu hizo; kuna ambao hawakufurahishwa na uamuzi huo na wapo wanaoona ni sawa kufanya hivyo.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu janja ya kwanza yenye "V" mbili
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.