fbpx

Samsung ya Ujerumani imetoa memori kadi ya 512GB

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tunafahamu vyema umuhimu/kazi ya kuwa na memori ya ziada kwenye simu hasa kama diski uhifadhi kwenye rununu sio wa kuridhisha (kulingana na matumizi) sasa Samsung ya Ujerumani imeongeza moja kwenye mtiririko.

Sio jambo la kushangaza kwa kampuni kubwa kuwa na matawi kwenye nchi mbalimbali na hii inaweza kusababishwa na sababu kadha wa kadha. Tumezoea kusikia bidhaa nyingi za Samsung zikitokea makao makuu lakini safari hii watengeneza memori kadi ya GB 512 kutoka tawi la kampuni hiyo nchini Ujerumani.

Memori kadi ya ukubwa wa GB 512 ina maana gani kwa Samsung?

Kampuni hiyo nguli kwenye biashara ilianza na memori kadi zenye ukubwa wa GB 32, 64, 128, 256 na sasa 512GB ambayo inawezo wa kupokea picha jongefu yenye ubora wa 4K ndani ya sekunde 38 tuu. Lakini kwa ukubwa huo ni sawa na kuhifadhi picha za mtato wa hali ya juu zenye urefu wa saa 78 au picha 150,300.

Samsung ya Ujerumani

Uwezo wa memori kadi za Samsung.

Kasi ya kutuma vitu memori kadi ya Samsung (GB 512) inafikia 100MB/sekunde na gharama yake ni $289|Tsh. 754,400 pamoja na kibali cha kuirudisha kitakachodumu miaka kumi lakini bado haijaingia sokoni.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Samsung Fold Kurudi Tena Sokoni Mwezi Wa 7!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.