fbpx

Serikali ya Tanzania yakanusha uzushi unaoenezwa mitandaoni

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari nchini kuhusu wanafunzi wanaohitaji mikopo ya elimu ya juu.

Madai ambayo yamekuwa yakisambazwa mitandaoni ni kwamba mwanafunzi yeyote ambae mzazi wake ana leseni ya biashara hataruhusiwa kupata mkopo kutokana na wazazi wake kuwa na uwezo.

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. William Ole Nasha amesema taarifa hizo si za kweli na amewaomba watanzania kuzipuuza kwani zina lengo la kuichonganisha serikali na wananchi wake.

uzushi unaoenezwa

Mitandao ya kijamii imekuwa njia moja rahisi ya kuwasiliana na watu popote duniani, muda wowote; zaidi ya watu milioni 4 wapo kwenye mitandao ya kijamii kwa Tanzania.

Mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya usambazaji taarifa mbalimbali kwa urahisi na haraka lakini inapotumiwa vibaya huleta usumbufu na madhara kwa jamii.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Facebook M: Facebook wanatengeneza 'Virtual Assistant'
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.