fbpx

Siku ya kwanza katika kongamano la TEHAMA 2018

0

Sambaza

Kwa mara nyingine tena wadau/wataalam wa masuala ya TEHAMA wameweza kukutana sehemu moja na kuweza kujadiliana mambo mbalimbali ambao yapo kwenye sekta hiyo.

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inakuwa kila leo na kwenye siku ya kwanza kwenye kongamano hilo tuliweza kufahamu takwimu mbalimbali:-

  • Watumiaji wa intaneti mwaka 2013 walikuwa mil. 3 lakini mpaka kufikia mwaka 2017 watu 27m wanatumia huduma ya intaneti ambapo ni sawa na 45% ya ukuaji kwa Tanzania, sawa na 36.1% kwa Afrka na 56.1% duniani kote,
  • Inaaminika mpaka kufikia 2020 zaidi ya watu biliono 20 watakuwa wanatumia intaneti.

Mengineyo yaliyojadiliwa kwenye siku ya kwanza katika kongamano la TEHAMA 2018.

http://spawaterway.com/shingles Sehemu ya TEHAMA katika jamii na umuhimu wake. Tanzania ambayo inaingalia teknolojia ya mawasiliano kwa ukaribu inaamini go here elimu sahihi ikitolewa na watu wakaelewa eneo hilo pekee litaweza kupunguza ukosefu wa ajira kwa 18% buy Lyrica europe lakini ni muhimu tujue kuwa 22.9% ya bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ni vifaa vya kidijitali.

INAYOHUSIANA  IPP kuanzisha kiwanda cha simu za mkononi nchini

Ujumuishwaji watu kwenye dunia ya kidijitali. Katika dunia ya leo ambayo ni ya kidijiti zaidi wahusika (watu) kwa asilimia kubwa inaonekana wapo nyuma/hawaendi sambamba na mabadiliko hayo hivyo kuathiri uchumi na watu wenyewe.

  1. Walemavu na vifaa vya kidijitali. Kama moja ya kundi maalum walemavu nao wana haki zote kutumia dijitali na kwa mfano mlemavu wa macho anaweza kutumia kompyuta/simu janja kama mtu mwingine hivyo basi kuweza kuachana na kuandika kwa maandishi ya nukta nundu badala yake kutumia kompyuta kufanya mengi zaidi kwa usaidizi wa programu ya sauti (NVDA-Non Visual Desktop Access).

    Siku ya kwanza

    Chuo Kikuu Huria Tanzania ni mfano wa kuigwa na makampuni/taasisi nyingine kwani inatumia teknolojia hiyo ikiwa na mtalamu kwenye idara hiyo.

  2. Majiji janja na matumizi ya intaneti. Nchi nyingi zinawekeza kwenye majiji janja ambapo kwa lugha rahisi kabisa ni maeneo ambayo yanatumia teknolojia ya juu kuweza kutumia teknolojia ya mawasiliano kufanikisha kitu fulani. Tanzania ina ndoto ya kuwa majiji janja lakini mambo hayawezi kufanikiwa iwapo hatutakuwa na umeme wa uhakika, upatikanaji nafuu sana wa intanetihivyo basi, ipo mipango ya kukamilisha utandazaji (kwa taifa zima) wa nyaya ndogo sana kwa ajili ya kasi ya intaneti.

Teknolojia nyuma ya sarafu za kidijitali. Makampuni kadha wa kadha yanawekeza kwenye sarafu zisizoshikika na hasa kwa kuanzisha sarafu zao wenyewe. Katika kipengele hiki ulitolewa utangulizi wa teknolojia husika, kwanini imetokea kuvutia mataifa mengi duniani na jinsi ya kuwekeza.

Mbinu za ufuatiliaji wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano. Matumizi ya TEHAMA katika dunia ya leo hayapingiki hata kidogo na kutokana na ukuaji wa teknolojia ni muhimu sana watu wakaeleweshwa sheria zinasemaje ili kutojikuta pabaya (mikononi mwa sheria).

Siku ya kwanza

Zipo sheria nyingi tu ambazo zinamlinda mtumiaji, aliyetengeza na hata serikali.

Jitihada za serikali za serikali kutumia teknolojia ya mawasiliano kuelekea uchumi wa viwanda. Mbali na kuwa na umeme wa uhakika, rasilimali watu, mashine pamoja na mengine lakini kamwe matumizi ya teknolojia hayawezi kubaki nyuma na ndio hapo ambapo serikali ikaweka wazi mipango yake katika kuhakikisha TEHAMA haibaki nyuma kufanikisha Tanzania ya viwanda.

Na hayo ndio yaliyoangaziwa katika siku ya kwanza kwenye kingamano la TEHAMA mwaka 2018. Tutaendelea kuleta mengi zaidi ili kuweza kukuhabarisha wewe msomaji wetu.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.