Ushindani kwenye biashara ya simu janja bado unaendelea kwa kuwa kila leo kuana simu rununu inatoka na kuiweka kampuni husika kutengeneza faida kutokana na bidhaa husika ikiwemo Realme 2 Pro.
Oppo inafamika ulimwenguni kwa vitu vyao na pengine ulikuwa ufahamu kuwa mbali na kutoa bidhaa zinazobeba nembo ya Oppo lakini kuna vitu vingine vinatoka mathalani Realme 2 Pro huku kampuni mama ni Oppo. Naamini unataka kujua simu hiyo ina sifa gani:
Kipuri mama+Muonekano.
Simu husika inatumia Snapdragon 660 ambayo ni moja ya vipuri mama ambavyo vina kasi na kuifanya simu kuvutia wakati wote. Kioo chake kina urefu wa inchi 6.3 kiwango cha ung’avu wa hali ya juu.
Kamera.
Realme 2 Pro ina kamera mbili upande wa nyuma; za MP 16 na nyingine 2 MP. Kwa mbele ipo kamera moja tu lakini ambacho kimenivutia ni ule muonekano wake.
Memori ya ndani+RAM.
Kipengele hiki kimenivutia sana hasa kutokana na aina tofauti tifauti za ukubwa wa memori; kuna yenye RAM GB/64GB diski uhifadhi, 6GB RAM/64GB memori ya ndani na GB 8 za RAM/128GB diski uhifadhi.
Betri+Programu endeshi.
Katika moja ya vipengele ambavyo huwa napenda kuvitolea macho kwa ukaribu ni uwezo wa betri kwenye simu husika. Realme 2 Pro inaelezwa kuwa na betri lenye 3500mAh ingawa haina teknolojia ya kuchaji haraka. Kuhusu programu endeshi ni Android 8.1.
Bei+Rangi.
Realme 2 Pro inaelezwa kuuzwa kwa $192|Tsh. 441,600 yenye 4GB RAM/64GB memori ya ndani, $220|Tsh. 506,000 kwa yenye 6GB RAM/64GB diski uhifadhi na $250|Tsh. 575,000 ambayo ina 8GB RAM/128GB memori ya ndani.
Upatikanaji wake unategemewa kuwa mwezi Oktoba katikati na bei zote zilizoainishwa ni za ughaibuni.
Vyanzo: GSMArena, India Today