Inapotokea mtu/kampuni iliyotengeneza programu fulani halafu ikawa inatoa masasisho baada ya kipindi kupita lazima iwepo sababu iliyosababisha jambo hilo kufanyika vivyo hivyo Slack imeboresha kitu muhimu.
Siwezi kushangaa iwapo mtu atasema kuwa hajawahi kujua/kusikia kuwa kuna programu iitwayo “Slack” ambayo inafanya kazi kwenye simu kama programu tumishi lakini pia kupitia kompyuta kupitia tovuti.
Slack ni nini?
Kwa kazi zinazojumuisha mawasilaino ya watu wengi/kampuni au taasisi na hawapendi kutumia maandishi kwenye karatasi mtakuwa mmeshaambiwa mtumie stack kufanya mawasiliano ya kiofisi.
Slack ni programu tumishi/tovuti ambayo inawezesha kundi fulani kwenye taasisi, kampuni, n.k kuweza kutoa mrejesho, kuuliza swali, kuchangia mawazo pamoja na mengineyo na wengine waliopo kwenye mfumo huo kuweza kusoma ulichokiandika.
Kitu kipya kwenye Slack.
Taarifa fupi fupi za kumhusu mhusika ni kitu muhimu hasa kutokana na majukumu mbalimbali au maudhui ya programu yenyewe ilivyotengenezwa. Sasa kilichoboreshwa ni kuweka muda ambao utakuwa unafanya kitu fulani; inaweza kuwa leo, kwa dakika 30, saa nzima, n.k. Baada ya muda huo kupita taarifa hiyo inapotea/kufutika.
Iwapo ninyi kama kikundi/kampuni hamjawahi kutumia Slack kupitia simu rurunu/kompyuta unaweza kuipakuwa kutoka App Store/Playstore mfurahie mengi zaidi kutoka huko.
Vyanzo: The Verge, Appcues