fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Intaneti simu Tanzania Tecno Tigo

Tigo Tanzania na Tecno wajisogeza karibu kwa wateja wake

Tigo Tanzania na Tecno wajisogeza karibu kwa wateja wake

Spread the love

Tecno ni moja kati bidhaa (simu janja) zilizoenea barani Afrika kwa wingi na kufanya kuwa na soko zuri barani humo lakini halikadhalika Tigo Tanzania nao wamekuwa wakijidhatiti ili kuweza kuendelea kufanya vizuri katika soko lenye ushindani na hatimae wasipoteze wateja.

Sote tunafahamu jinsi gani Tigo Tanzania ilivyokuwa na wateja wengi na kuzidi kuendelea kuwavutia watu wengine kila siku. Hivi karibuni Tigo Tanzania na Tecno wamua kushirikiana kwa faida ya wao na wateja wa bidhaa zao.

SOMA PIA  Maana ya "TTY Mode" kwenye rununu

Siunafahamu simu janja mpya ya Tecno Camon X? Basi Tecno na Tigo Tanzania wanasema kwa kila mteja atakayenunua simu hiyo atakuwa anapata GB 3 za kifurushi cha intaneti BURE kila mwezi kwa muda wa miezi sita.

Tigo Tanzania na Tecno

Wawakilishi kutoka Tigo Tanzania na Tecno wakiongea na waandishi wa habari kueleza umma watakachokuwa wakifanya.

Ambacho pengine hukifahamu……

Tecno wameamua kufanya kazi na Tigo Tanzania kwa sababu ya Tigo kuwa na intaneti ya 4G katika maeneo mengi nchini humo (Tanzania) na isitoshe simu ya Tecno Camon X ina mfumo wa 4G hivyo kufanya wateja wake kufurahia intaneti yenye kasi kutoka Tigo Tanzania.

Tigo Tanzania na Tecno

Simu janja ya Tecno Camon X

Tigo Tanzania ndio kampuni ya ya kwanza ya mawasiliano kuweza kuleta simu hizo katika maduka yake yote yaliyopo katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Vilevile, mteja anaweza kununua simu janja ya Tecno Camon X kwa kulipa kidogo kidogo; unapiga *147*00# kisha utafuata maelekezo au kununua kupitia MTANDAONI.

Tecno Camon X inauzwa Tsh. 469,999 katika maduka yote ya Tigo ambapo simu hiyo itakuwa na kifurushi cha GB 3 za bure kila mwezi kwa siku 180. Bofya HAPA kujua sifa ya simu hiyo pamoja na mengineyo.

Chanzo: Tigo Tanzania

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania