fbpx

Twitter ujumbe kuwa na tiki za kusomwa kama WhatsApp na Facebook Messenger

0
Sambaza

Mtandao wa kijamii wa Twitter umefanya maboresho katika eneo lake la kuchati ambayo wengine wameyapokea vizuri na wengine wanaonekana hawajapendezwa nayo.

Twitter walitangaza mabadiliko hayo kupitia akaunti yao ya Twitter na pia blog yao.

twitter ujumbe kuwa na tiki

Muonekano wa eneo la mipangilio (settings) za Privacy

where to buy viagra in stores Mabadiliko/boresho hayo

  • Ujumbe kuwa na tiki. Mtumaji wa ujumbe kupitia eneo la kuchati (direct messaging – DM) ataweza kuona kama ujumbe wake umesomwa au la.
  • Utaweza kujua kama unayechati naye anakuandikia majibu kwa wakati huo au la – (typing indicators)
  • Pia utaweza kuona taarifa fupi za tovuti flani pale mtu anavyokutumia linki flani – (web preview)
INAYOHUSIANA  Ifanye WhatsApp isichukue nafasi kubwa

follow site Kwa kiasi kikubwa hili linaonesha Twitter nao wanataka wazidi kutambulika kama eneo la mazungumzo ya kuchati kama vile zilivyo app za WhatsApp na Facebook Messenger.

Twitter imejikuta katika hali ya ukuaji wa kasi ndogo sana katika miaka ya hivi karibuni na inaonekana tutaendelea kupokea taarifa za mabadiliko na maboresho mbalimbali wakijitahidi kuvutia watumiaji wapya.

Je wewe ni mtumiaji wa Twitter? Je umependa maboresho hayo?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.