Tulikua tumeshazoea ile hali ya kwamba tunatumia App ya Uber katika simu zetu na tunaita usafiri ambao unatuhusu moja kwa moja lakini kwa sasa kuna mabadiliko
Kipengele hiki kipya kutoka Uber kinatoa kipaumbele kwa watu ambao wanaelekea uzeeni yaani wale wa miaka 65 na kuendelea.
Inasemekana kuwa asilimia kumi ya watu duniani ni wazee na jambo hili kampuni ya Uber imeliona na ndio maana imeamua kuja na kipengele hiki
Lakini kwa upande mwingine sio kwamba toleo hili ni kwa ajili ya wazee tuu bali hata marafiki wa kawaida na ndugu unaweza ukawaitia Uber
Kitu kinachofanyika ni kwamba wakati unaomba Uber kutatokea na chaguzi likikuuliza kwamba Uber hiyo ije kwako au iende kwa rafiki au ndugu. Ukichagua chaguo la rafiki au ndugu basi itakubidi uchagua namba ya huyo rafiki katika ‘phonebook’ na kisha Uber itamtumia meseji mtu huyo ambayo ‘link’ ambayo itamuwezesha kufuatilia usafiri huo wa Uber. Taarifa kama nani analipia huduma hiyo na aina ya gari linalokuja vyote vinakua ndani ya meseji hiyo.
Hili ni jambo zuri sana fikiria wewe unaweza ukawa upo Dar lakini ukamuita Uber mtu wa Morogoro na ukalipia kila kitu wewe. hii imekaa poa!
Ningependa kusikia kutoka kwako, hili jipya kutoka Uber unalionaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment.
Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.