fbpx

Udhaifu wabainika kwenye mtandao maarufu wa kijamii

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mitandao ya kijamii imekuwa moja ya vyombo mbalimbali ambavyo vinatuwezesha kufikia watu wengi sehemu nyingi duniani kutokana na ukuaji wa teknolojia na intaneti kwa ujumla.

Facebook umekuwa mtandao wa kijamii ulio na watumiaji wengi kila siku na hali ilivyo sasa kutokana na kurahisishwa namna ya kujiunga na Facebook basi si jambo la kujiuliza mara mbili mbili nikisema Watu wengi wanatumia mtandao wa kijamii (Facebook) zaidi ya hata mara kumi na tano kwa siku“. Ni kweli, si ndio?

Katika utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Iowa na Lahore Management imebainika Facebook inasumbuliwa na kuwa na watumiaji ambao si halisi na matokeo yake unakuta habari fulani imependwa na watu mil. 1 kumbe habari hiyo imependwa na akaunti ambazo si halisi.

Kashfa kama hiyo si mara ya kwanza kwa Faceook kwani mwaka 2016 katika uchaguzi mkuu wa Marekani Facebook ilihusishwa kueneza habari zisizokuwa za kweli katika kipindi hicho cha uchaguzi na kwa namna fulani kusukuma rais aliye madarakani nchini humo kushinda.

Akaunti hizo zimebainika kuwa zina uwezo wa kujiunga na Facebbook na kuweza kutoa maoni/kupenda kitu fulani na kupelekea habari fulani kupendwa na watu hatu mil. 100 kumbe si kweli.

Uwepo wa akaunti hizo ambazo si halisi unaweza kusababishwa na mchapishaji wa habari husika kwenye Facebook kwa lengo la kujinufaisha kwa namna moja au nyingine. Sijui wewe una mawazo gani, tuambie hapo chini katika sehemu ya kutoa maoni.

Vyanzo: Fortune, CBS News

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Facebook kuja na sarafu yake ya kidijitali mwaka 2020
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|