Tulishaandika kuhusu ujio wa huduma ya usafiri wa Uber Tanzania miezi michache iliyopita. Sasa ni rasmi, huduma ya usafiri ya app ya Uber yaanza rasmi kutoa huduma zake jijini Dar es Salaam.
Kupitia vyanzo mbalimbali pamoja na kwenye mtandao wao ni rasmi sasa unaweza kupata huduma ya usafiri wa kukodi kwa urahisi zaidi sasa kupitia app ya Uber.
Uber ni huduma inayounganisha watu wenye magari ya aina mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na taksi (Taxi) katika kuweza kutoa huduma kwa urahisi na kwa bei inayoeleweka kupitia app ya Uber.
Kupitia mtandao wao gharama za usafiri wa huduma ya Uber kwa sasa kwa maendeo ya jiji la Dar es Salaam upo kama ifuatavyo;
- Malipo ya kwa dakika – Tsh 95.00/=, hii inaweza usisha gharama ya kusubiriwa n.k
- Malipo ya kwa Kilometa – Tsh 466.03 (badala ya kukisia kisia bei kama ilivyo kwa sasa, magari ya huduma ya Uber yatakuwa na kifaa cha kuhesabu umbali wa safari yako na hivyo utalipa kutokana na kilometa za safari yako)
Bei ya chini kabisa ya safari moja ni Tsh 3,000/=, yaani ata kama kwa KM ulizotembea ni chini ya gharama hii lazima utoe kiasi hichi. Pia pale utakapokuwa umeita usafiri kupitia app hii na kisha ukaamua kuhahirisha, yaani ‘Cancel’ basi utakatwa faini ya Tsh 3,000/=.
Huduma ya Uber inaruhusu pia watu mbalimbali wenye magari yanayoweza kutumika kwa usafiri wa kukodi kujiunga nao. Hivyo kama una kagari cha maana basi unaweza kujiandikisha na kuchagua masaa ambayo unaweza kutoa huduma ya usafiri.
Je mfumo wa usafiri wa Uber unafanyaje kazi?
Usafiri wa Uber ni usafiri unaowaunganisha watu wanaoitaji usafiri na madereva taxi, na ata madereva wa magari spesheli – ya hali ya juu na ya kuvutia.
Kupitia app yao utaweza kuwa na akaunti yako, kupata taarifa kuhusu madereva waliokaribu yako, kuita dereva, kuona gharama ya usafiri kupitia app hiyo na ata kulipa kupitia akaunti yako ya benki/Paypal uliyounganisha ndani ya app hiyo na kwa Kenya unaweza kulipa ata kwa kutumia huduma za kibenki za simu (kama vile Mpesa, Airtel Money n.k) kitu ambacho kinaweza kuwezesha kwa Tanzania pia.
Kwenye baadhi ya mataifa huduma hii imekuwa ikipata changamoto kubwa kutoka kwa madereva taksi ambao wanakuwa wagumu kufahamu faida ya huduma hii na kujiunga kwa upesi.
Kwa sasa usafiri unapatikana kupitia aina ya magari yaliyopewa jina la UberX, haya ni ya bei nafuu…ila haitachukua muda kuona magari ya bei ghari zaidi kuanza kupatikana na haya yatakuwa na bei tofauti.
Chanzo/Pia kubook usafiri -> Uber/Dar es Salaam
Download/Pakua app ya Uber -> Google PlayStore | AppStore(iOS)
One Comment
Comments are closed.