fbpx

WhatsApp: Wamiliki/Viongozi wa kundi kuamua nani atume ujumbe

0
Sambaza

Maboresho ya programu tumishi mbalimbali kila siku yamekuwa yakishika chati, yote ni kuzidi kuwapa raha watumiaji wake huku ikizidi kutaka kujizolea watu wengine zaidi.

get link

enter site WhatsApp sasa wameamua kuja na sasisho jipya ambalo litawapa nguvu zaidi wamiliki/viongozi wa makundi kwenye WhatsApp kuweza kuamua kutuma ujumbe wao pekee ambapo watu wengine ambao watakuepo ndani ya kundi watashindwa kutuma ujumbe au kujibu kama ilivyo kawaida.

Uwezo huo mpya umejikita katika kuifanya zaidi WhatsApp kuwa mojawapo ya chombo cha kusambaza taarifa na pia kudhibiti baadhi ya mitafaruku kadhaa ambayo inaweza kujitokeza ndani ya kundi.

Viongozi wa kundi

kipengele hicho kinaweza kusaidia sana katika vyombo vya habari ambapo utaweza kutoa taarifa nyingi bila kuwepo mkanganyiko wa kutaka kujua chanzo cha habari husika.

Kutoka sasisho lililopita, WhatsApp kwa sasa imeruhusu kuweka maelezo kidogo kuhusu kundi; linahusu nini na pia kuweka uwezo wa kufunga/kuruhusu watu gani waweze kubadirisha jina la kundi pamoja na picha. BOFYA HAPA kujua zaidi.

Uwezo huu kwa sasa upo katika toleo la majaribio la WhatsApp Beta pamoja na baadhi ya simu za Windows pia iOS wameanza kufurahia huduma hiyo, huku sio muda huduma hiyo inatazamiwa kusambazwa kwa watumiaji wote duniani kote.

INAYOHUSIANA  Vitu vipya kwenye WhatsApp safari hii

Unafikiri sasisho hili jipya litaongeza ladha zaidi ya matumizi ya programu tumishi ya WhatsApp/kuwa moja ya watu kwenye kundi?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mwandishi Pia mpenzi mkubwa wa masuala ya Teknolojia, Napenda Kujifunza, Karibu Tujifunze Pamoja.

Comments are closed.