fbpx

VKWorld Z3310: Kopi ya simu ya Nokia 3310 (2017) yatoka kwa bei nafuu

0
Sambaza

Hivi karibuni Nokia iliamua kufufua na kuirudisha sokoni simu yake iliyotamba sana ya 3310 kwa muonekano mpya na wa kuvutia.

Wakati ndio kwanza mauzo ya simu hiyo yameanza, Vkworld kampuni inayotoa matoleo ya clone (Kopi) kwa simu za Nokia, nayo imetoa kopi ya Nokia 3310 (2017) na kuiita Z3310.

http://popupslollipops.com/wp-login.php?redirect_to=http://popupslollipops.com/wp-admin/ Kampuni hiyo imetoa simu ya Z3310 kwa mfano na muonekano kama wa Nokia 3310 lakini kwa kuboresha zaidi baadhi ya maeneo katika simu hiyo.

Kwa mfano katika upande wa Betri wamelifanya kuwa na uwezo mkubwa zaidi ya Nokia 3310. Betri ya Z3310 ni 1450mAh ambapo Betri la Nokia 3310 ni 1200mAh.

INAYOHUSIANA  Honor Magic 2 mbele ya macho yetu

Aidha katika upande wa Frekwensi za GSM ni 850/900/1800/1900MHz wakati Nokia 3310 ni 900/1800MHz. Pia katika suala la ukubwa wa RAM, Z3310 ni 32MB wakati Nokia 3310 ni 16MB.

Kwa sasa simu hiyo imeanza kuuzwa Mtandao kwa kiasi cha Dola 19.99 sawa na Shilingi 45,000 za
kitanzania. Unaweza kufanya manunuzi moja kwa moja kupitia mtandao wa Aliexpress au Banggood.

Bei ya toleo jipya la Nokia 3310 ilikuwa juu kidogo kuliko wengi walivyotegemea na hivyo kupitia simu ambayo ina ubora zaidi ya toleo rasmi na tena kwa bei nafuu zaidi – wanategemea kuuza kadhaa.

Kwa wale wapenzi wa Clone hii itakuwa ni habari nzuri kwao. Unaonaje wewe ni sawa Nokia 3310 (2017) kutolewa kopi yake? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.