fbpx

WhatsApp kupambana na taarifa za uongo

0
Sambaza

Tatizo la usambazaji wa taarifa zisizo za kweli mitandaoni limeendelea kuisumbua WhatsApp kiasi cha kuanza kuweka udhibiti maalum wa kuendelea kusambazwa kwa habari za uongo.

buy aromasin and nolvadex

Watumiaji wa WhatsApp karibuni wataanza kuwekewa udhibiti idadi ya kutuma ujumbe wanaowasambazia watu wengine pamoja na makundi mbalimbali ya WhatsApp.

Taarifa iliyotolewa na WhatsApp wenyewe inasema watumiaji wataweza kusambaza jumbe 20 tu huku nchi kama India wakiruhusiwa kusambaza takribani jumbe 5 tu.

taarifa za uongo

Hatua hii imekuja baada ya watu kadhaa kupigwa na wengine kuuawa kwa sababu ya taarifa za uongo kusambazwa kupitia njia ya ujumbe wa WhatsApp.

Nchi za India, Myanmar na Sri Lanka zimeripotiwa mara kadhaa kukumbwa na mauaji, utekaji uliosababishwa na jumbe za uongo za WhatsApp.

Mfumo wa ujumbe wa WhatsApp wa ‘ accutane purchase online uk end to end encryption‘ umewafanya WhatsApp wenyewe kutojua kinachotumwa hivyo kushindwa kuzuia ujumbe wa uongo unaosambazwa kupitia programu tumishi ya WhatsApp.

WhatsApp imeahidi kuendelea kudhibiti taarifa za uongo, huku India yenye watumiaji milioni 200 wa WhatsApp ikiongoza kwa usambazaji wa habari za uongo ikifuatiwa na Brazil.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kutuma jumbe za kawaida kupitia tovuti
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.