Unapotaka kitu kivutie basi jambo ambalo unaweza kufikiria ni kuboresha kila mara unapoona kuwa kuna umuhimu wa kufanya hivyo vivyo hivyo WhatsApp na machapisho ya picha mnato kutoka Facebook na Instagram.
Katika makala zangu kadha wa kadha zinazohusu masasisho kwenye WhatsApp huwa nashauri sana watu waweze kutumia toleo la WhatsApp BETA na hii ni kwa sababu kuu moja tu; masasisho yote yanayohusu programu hiyo huwa yanaanzia huko kabla ya kuruhusiwa kwa wengine.
Kwa wanaotumia toleo ambalo ni la majaribio kwenye WhatsApp (Beta v2.18.301) wanaweza kucheza picha jongefu zilizotoka kwenye machapisho ya Facebook au Instagram bila kupelekwa sehemu ambapo picha mnato imechapishwa.
Kwa wanaotumia iOS ambacho kimefika kwenye Android sio jambo geni kwao kwani ilianzia huko kabla ya kuletwa upande wa pili.
Masasisho hayo bado hajaanza kupatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp kwenye Android na hata picha mnato kutoka Twitter zitafunguka kwenye uwanja tofauti (sio kama za kutoka kwenye Facebook au Instagram).
Vyanzo: GSMArena, Android Police