fbpx
apps, whatsapp

WhatsApp yatoa seti ya emoji zake mpya katika Toleo la WhatsApp Beta v2.17.364

whatsapp-yatoa-seti-ya-emoji-zake-mpya
Sambaza

Kwa muda mrefu WhatsApp imekuwa ikitumia Emoji za Apple lakini sasa imeamua kuja na seti yake yenyewe kama baadhi ya makampuni mengine ikiwemo Twitter.

Ingawa kuna utofauti mdogo ila bado muonekano wa emoji za WhatsApp zinafanana kwa sana na zile za Apple, kwa zoezi la kuja na seti zake za Emoji basi wengi walikuwa wakitegemea utofauti mkubwa.

WhatsApp yatoa seti ya emoji zake mpya
WhatsApp yatoa seti ya emoji zake mpya: Juu ni emoji zilizokuwa zikitumika kwenye WhatsApp zamani, na chini ni muonekano wake mpya

Kuna Emoji mbalimbali kama wafanyakazi wa ujenzi, mimea, magari, Wanyama, ndege, Matunda nk. Kinachoonekana WhatsApp wameamua kuchukua Emoji za Apple na kufanya marekebisho kidogo.

INAYOHUSIANA  Facebook Messenger: Kuja na 'Option' ya kufanya mazungumzo baina ya mtu na mtu kuwa salama zaidi

Kwa sasa Emoji hizo zimeanza kupatikana katika katika WhatsApp Beta toleo la v2.17.364. Taarifa zinasema aidha zinaweza kuongezwa au zingine kupunguzwa kabla ya kuwafikia watumiaji wote wa WhatsApp.

Emoji za upande wa kulia ndio mpya za WhatsApp
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.