Tangu wiki iliyopita, WhatsApp imekuwa ikipatikana kwenye kompyuta kupitia kivinjari cha Google Chrome. Huu ni mwanzo tu, huduma hii itasambaa kwenye Firefox na vivinjari vingine katika siku za karibuni.
Kuna njia mbili za kufungua WhatsApp kwa haraka zaidi kwenye kivinjari cha Google Chrome: Kupitia ‘Bookmarks’ (kumbukumbu) na kupitia njia fupi zaidi ya kuweka ‘short-cut’ kwenye ‘task-bar’, start-menu na kwenye desktop pia.
Kupitia Bookmarks
Uwapo kwenye web.whatsapp.com, bonyeza ‘ctrl’ + ‘D’na katika kisehemu cha Jina weka whatsApp. Unapoandika WhatsApp tena kwenye kisehemu cha anuani, Google Chrome itakumbuka kurasa ya whatsapp na kukupa urahisi wa kuifungua app hiyo.
Tazama picha hapa chini.
Kupitia Shot-kati
Kupitia Shot-kati ya kwenye ‘taskbar’, ‘task-bar’, start-menu na kwenye desktop:
Ingia web.whatsapp.com. Uwapo kwenye kurasa hii, fungua ‘menu’ ya Chrome na shuka hadi kwenye zana zaidi (‘more tools’) na chagua ‘unda mikato ya programu’ (‘create application shortcuts’). Kisha chagua unataka shoti-kati yako ikae wapi kati ya Eneo-kazi (‘Desktop’), Menyu ya Kuanzia (‘Start menu’) au upau wa shughuli (‘task-bar’). Fuatilia picha hii hapa chini.
No Comment! Be the first one.