Masihara yaweza kuwa dhihaka lakini pia utani una faida zake mbali na kukufurahisha na kuongeza siku za kuishi duniani kiasi cha kumuwezesha askari mmoja nchini India kupatiwa matibabu.
Taarifa ya Twitter iliyotumwa na mwandishi maarufu wa India kumuaibisha polisi mmoja wa nchi hiyo kwa kuwa mnene kupindukia imekuwa na matokeo ambayo hayakutarajiwa; kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito mjini Mumbai bila malipo yoyote.
Mwandishi alituma ujumbe wa Twitter wa picha ya Bwana Jogawat mwezi uliopita, akisema kuwa polisi huyo aliyeko Mumbai alikuwa na mpango wa “kuweka usalama mzito” kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Ujumbe huo uliosambazwa sana na kupelekea hospitali ya Saifee kujitolea kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wake.
Insp.
alipata fursa ya kwenda Mumbay kwa mara ya kwanza ajili ya matibabu kwa sababu ya ujumbe wa Twitter na kuongeza kuwa uzito wa mwili ulianza kuongezeka kutokana na matatizo ya kiafya, na si kwa sababu anakula sana.Inspekta Jogawat anaendelea vema baada ya upasuaji, na uzito wa mwili wake unaweza kupungua hadi karibu kilo 80 katika mwaka ujao. Alikuwa na uzito wa kilo 180 kabla ya upasuaji.
Vyanzo: BBC, The Financial Express