Oracle watalazimika kuilipa zaidi ya Tsh 6.6 trilioni kampuni ya “Hewlett Packard (HP)” baada ya kushinda kesi dhidi ya Oracle kwa madai ya kuacha kutengeneza software kwa ajili ya Itanium processors.
Baada ya hapo Oracle walikataa kutengeneza programu wezeshaji(software) yenye kuweza kufanya kazi kwenye servers zinazotumia “Itanium chips” na kusababisha HP kupata hasara kutokana na Oracle kukataa kutengeneza software hiyo.
Mwaka 2012 Oracle iliamuliwa na mahakama kuendelea kutengeneza software hiyo kwa ajili ya servers lakini amri hiyo haikusaidia kwani tangu mwaka 2011 HP walikuwa wameshaathirika kutokana na kuachwa kutengenezwa software hiyo.
Inaaminika waliacha kutengeneza kwa sababu ya kuvutia wateja kununua hardware (kompytuta, programu wezeshaji, n.k) inayotengenezwa na ‘Sun’ kampuni inayomilikiwa na Oracle.
Intel iliacha kutengeneza Itanium chips na kufanya kampuni kuamua kutumia kompyuta zenye uwezo wa hali ya juu sana(servers) zinazotengenezwa na makampuni mengine kama Sun ya Oracle.
Oracle haikuwa na jukumu la daima kuendelea kutengeneza programu hiyo wezeshaji kwa ajili Itanum processors hivyo waliamua kufanya hivyo kutokana waliona kuwa bidhaa hiyo ilikuwa imeshaanza kukosa soko ndio maana wakaacha kutengeneza software hiyo.
Ingawa HP wameshinda kesi hiyo tangu mwaka 2012 lakini kiasi hicho cha fidia imeamuriwa hivi karibuni. Oracle wamesema watakata rufaa kutokana na uamuzi huo wa mahakama. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Oracle kushindwa kesi dhidi yake baada ya kushindwa kesi dhidi ya Google na kuiliwa jumla ya dola bilioni 9.
Je, unadhani Oracle kuendelea kushindwa kesi dhidi yake itashusha heshima ya kampuni hiyo na hatimaye kuweza kufilisika hapo baadae? Tuambie katika comment hapo chini. Teknokona tunakuhabarisha kama kawaida yetu kwa lugha ya Kiswahili.
Chanzo: BBC, Tech times, Reuters